chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 16,859
- 28,112
Kuna mahali naona hapako sawa, ili uwe mbunge Tanzania ni kujua kusoma na kuandika, kwa maana kwamba hata darasa la nne anaweza kuwa mbunge, na pengine hata kingereza akawa hajui, inakuwaje anamsikiliza mtahiniwa/msailiwa kwa lugha ya kingereza wakati yeye haijui?halafu baada ya hapo anapiga kura? Anakuwa ameelewa mgombea kaongea nini?