Wabunge wa CCM kuna wakati wanachekesha sana, Hamis Taletale atoa msaada wa taulo za kike kwa wanafunzi

Kwani kutoa Taulo za Kike ( Sanitary Towels / Pads ) kwa Mabinti wa Shule wenye Changamoto za Kiuchumi katika kuzipata siyo Jambo jema na hata la Ustawi wa Kimaendeleo kwa Wanafunzi hao?

Siku hizi Uwezo wako wa Kujenga Hoja unaanza Kupungua sana na sijui umekumbwa na nini. Nilidhani kwa hili ungempa Kongole ( Pongezi ) Mbunge huyu ( huyo ) matokeo yake umekuja Kumkandia ( Kumsiliba ) huku ukiona hakuna lenye Tija na Mantiki alilolifanya.

Waswahili bhana!!!!!!!
 
Hivi umasikini utaisha lini Tanzania na kila mpiga kura ni masikini na kibatizwa myonge. Hi Tabia naisikitikia sana Tengeneza Tatizo tatua tatizo ili uinekane wa maana.
hakuna nchi isiyo na masikini duniani
 
sizani kama umenielewa, kwani nimesema huwa wanashindwa kwenda shule? Nimesema wazazi hawana uwezo wa kuwanunulia watoto pedi kila mwezi hivyo mana kwanza unakuta mtu ana watoto 3 au 4 wakike ni ngumu kuweza kumudu kuwanunulia pedi kila kwenzi, hao watoto inawalazimu kutumia vipande vya vitambaa ambavyo kiukweli vinaweza visiwe salama sana kwa afya yao ya viungo vya uzazi kulingana na kwamba unahitajika usafi wa hali ya juu kuvitunza hivyo vitambaa, Pedi ni salama. Alafu huwezi kulinganisha msaada wa pedi na wa kujenga librabry, kwahiyo kama hana uwezo huo ndo asitoe msaada kabisa?
 
Sifa za mbunge.
Ajue kusoma na kuandika. Kwa level gani haijulikani.
 
Mbona miaka hii taulo za kike imekuwa ni issue kuuubwa, kwani miaka ya huko nyuma wadada na wamama walikuwa hawapati hedhi?
 
Badilika mkuu wajali watoto wa kike
Kweli tubadilike mkuu,ila najiuliza Mimi kama Mimi sijawahi kuwaza hata Siku moja kwamba watoto wadogo wa kike wako desperate na taulo.

Nikiwa kama mwanaume,hata hapa nyumbanj kwangu sijui ananunua vipi though hela ya matumizi namwachia mamaye.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…