Uchaguzi 2020 Wabunge wa CCM na waliohamia CCM, walioangushwa kura za maoni 2020

Muda muafaka wa kwenda kujiajiri na kupata first hand experience ya maazimio mbalimbali waliyokua wanayapitisha huko mjengoni.

Wakawekeze sasa kwenye viwanda, kilimo na ufugaji bila kusahau ktk teknolojia.

Ila wasihofu sana, mambo yakiwa tight wapeleke CV zao kwenye mojawapo ya maelfu ya viwanda walivyokuwa wanaambiwa vimeanzishwa na wao wanagonga meza huku wanachekaaaa.

Ombi kwa Mwenyekiti chonde, chonde wasipindue meza kila mtu avune alichopanda.
 
Ilikuwa hakuna namna kwa Albert Obama (Manyovu) na Nsansugwanko (Kasulu) maana wale wateule wa Rais (Dr. Mpango & Prof. Ndalichako) walikuwa ni lazima wapite hata kwa grader.

Juma Ngamia sasa akapige goti kwa JPM japo amdondoshee uDAS kabla ya Uchaguzi
 
Sijamuona mbunge wa Nkasi Kusini nasikia naye kaangukia pua. Hebu fuatilia mkuu.
 
Ni vyema walivyoangushwa, tena hao ambao walikuwa wanaunga juhudi za mwenyekiti wa chama imekuwa ni zaidi ya furaha kwa kweli walivyopigwa chini.
Hapo ndo itafahamika kama walikuwa wanaunga juhudi toka moyoni au walikuwa wanaunga juhudi kwa ajili ya matumbo yao.
 

Karibuni mtaani tugombanie ajira zilizopo.
 
Wapumzjike ili wengine nao waende....
 
Kwa kiasi kikubwa hawa wangeenda shusha heshima ya bunge likaonekana dhaifu kuliko lililopita kwa kutetea maagizo badala ya taifa.
 
Ungeweka katika mchanganuo wa kuunga mkono juhudi na wale asili. Mfano Mwakyembe ni yupo kundi la asili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…