Tetesi: Wabunge wa CCM Waanza Kutishiwa!

Kimsingi jamaa naona kafanikiwa sana kuubana upinzani na kuuzofisha kwa kiasi kikubwa
 
wanachoniacha hoi wabunge wa ccm, wanapiga hoja baadae na mwishoni ati naunga mkono, kweli woga umewatawala sana
 
Cc tulio huku chini ndio tunaona move. jamaa wako busy sana kujenga chama mashinani. kadi zinauzwa kama pipi. kama wakienda HV 2020 ssem watashangaa
 

Acha Blaa blaa za kusingizia CCM , Wewe sasa ndio Ujiulize kwanini Salum Mwalimu kapata kura nyingi za Ukawa kuliko za hao uliowataja?

Umewahi kujiuliza kwanini kati ya hao uliowataja Hakuna aliefikisha walau kura 50 wakati Ukawa peke Yao wanakadiria 100?

Masha na Wenje baada ya Uchaguzi kurudiwa kura walizopata hazifikii hata nusu ya kura walizopata awali huoni kuwa hilo ni jibu tosha hata ndani ya Chama ilishinikizwa tu kuwachagua na baada ya options kuongezwa na kuruhusiwa kupiga kura kwa Siri pale mbele wengi wa Wabunge wa Ukawa waliwakataa?
 
Bashe na Nape walishapigwa X na Bashite Sr. tangu Juzi. Mwingine ni Kitwaga ila yeye atabembelezwa na Ubalozi au Kitu cha aina hiyo!
Du kweli kuna plan yaani yote hayo ili mradi Kitwanga aachiei jimbo kwa mtoto kipenzi
 

Shida yako Ulikimbia umande Walikuwa Jumla ya Wagombea 6 hata tukisema kila mtu alipata kura sawa kutoka Chadema wote wangepata Kura 17 hivi kwa hiyo zingine zote zilitoka CCM. Sasa wewe Point yako ni nini? Maana hata uanchoongea hakieleweki wana hata wewe hukielewi!
 
Tujiulize ni Kwanini Magufulialikimbia Msiba Arusha kwa Kuogopa Kufunikwa na Lowassa?. Maana msidhani huo ujanja wakitoto wa kubadilisha hoja hatuujui. Tunaongelea Mengine mnataka kuleta Destruction!
 
Mkuu TL Marandu, ninakusoma in between the lines na ninakuelewa sana.

Hili la Chadema kuwa sikivu na kusikiliza ushauri ni jambo la msingi sana!.

Ili chama cha upinzani kiweze kwenda ikulu baada ya kushindwa uchaguzi uliopita, lazima kwanza kiangalie kilipojikwaa na kusababisha kuanguka, na sio kuangalia tuu kilipoangukia, kuamka na kuendelea na safari, kupitia njia ile ile na kikifika pale pale kilipojikwaa mwanzo, kitaendelea kujikwaa na kitaanguka tena na tena!.

Hatua ya kwanza baada ya kushindwa ni kufanya tathmini umeshindwa wapi, umeshindwa nini, umeshindwa vipi!.

Hatua ya pili ni kumpumzisha kiongozi mkuu no matter how good he/she is!. Chama kikiishashindwa uchaguzi mkuu lazima Mwenyekiti apishe damu mpya!.

Ile 2010 baada tuu ya uchaguzi, nilitoa ushauri huu kwa Chadema...

CCM Imechokwa, CHADEMA Haijajipanga!

Mtazamo: Kanda ya Kaskazini, CCM imechokwa mpaka basi!

Kuelekea 2015: CHADEMA, Don't Miss the Target, Adui Mkubwa sio CCM Bali ni .....!

Kama Chadema wangenisikiliza ushauri hug, amini usiamini Chadema saa hizi wangekuwa Ikulu!.

Paskali
 
ukiwa mbunge wa ccm unapaswa kuwa jasiri sana ili kutetea wananchi wako. nje ya hapo utabaki kuwa ni mbunge wa chama.
 

Sasa Wewe usiekimbia Umande hujui kuwa Chama chako hakikuwa na strategy ndio sababu hawakukubaliana kura wampe Nani au Wabunge wenu walisaliti Maelekezo ya Ayatollah Mbowe!

Wagombea wote ni wa Chadema na wameletwa na Chadema halafu CCM ikitumia Demokrasia yake kuchagua inaoona Wanafaa mnakuja kulaumu CCM wakati Nyie ndio mliowaleta mkiaminisha Bunge kuwa ndio wanafaa!

Kitendo cha Kura za Wenje na Masha kupungua ukilinganisha na Mara ya kwanza na kufikia Wenje baada ya marejeo kushika Mkia inaashiria hata ndani ya Chama walikuwa hawakubaliki
 
Ila kweli hapo chadema walifanya mistake.
 
Pascal 2015 Chadema walishidwa kwa kuhujumiwa na pamoja na kuhujumiwa huko bado waligain sana kwenye wabunge. Hivyo sioni kama Mwenyekiti akibadilishwa itasaidia. Hujuma aliyopanga kuwafanyia Magufuli 2020 ni mbaya zaidi. Kama wana akili wanatakiwa Nao watumie fedha, Intelligence etc Wamfanyie Hujuma mara mia zaidi. Tena sio wangoje 2019 watakuwa wamechelewa wanatakiwa waanze sasa.

Inashangaza Sana CCM ambayo Ilinyang'anya Computer za UKAWA za Parallel Tabulation sasa wao Ndio Wamemsaidia Raila Odinga na ODM kuweka Kituo cha Computer Tanzania. What an Irony. Mimi naomba sana Uhuru ashinde Ingawa simtaki Ruto lakini Kama UKAWA wana akili wangekopa hata pesa kwa Uhuru Kujiimarisha Kimkakati na Kumfanyia Magufuli hujuma mara mia zaidi ya anavyowafanyia yeye. Inahitajika kiasi cha kama Bilioni 10 hivi za Tanzania ambazo ni Kama million 90 tu za kenya na ni dollar kama Million 4 hivi. CHADEMA wakiwa na Kiasi hiki wakakiweka kwenye Intelligence na Operations CCM itahenya 2020. Na sio Kiasi Kikubwa Lowassa anaweza Kuwasaidia Chadema Kupata Mkopo au Msaada Huo kutoka kwa Uhuru!
 
Bye! Jiulize Kwanini Magufuli alikimbia Msiba kwa Kumwogopa Lowassa kama anajiamini? Anamwogopa mpaka Kupeana naye Mkono anauita ni Muujiza! Wongo kweli?
 
Hao wanaChama watawaongeZa mda gañ Na hali baba yak0 kafinya uhuru wa siasa.?TUMIA
Ub0ngo
wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…