Nani kakuambia tunaona aibu?
Hata mimi nimemshangaa sana. Tangu lini CCM mkawa watu wa kuona aibu!!? Yaani amewakosea adabu kupitiliza. Na kama vipi awaombe radhi huku akiwa amepiga magoti.
CCM HUWA HAMUONI AIBU
Mambo mangapi ya hovyo mnafanya na hamjawahi kuona aibu.
Hamkuona aibu kupora uchaguzi ndiyo mje muone aibu bungeni?
Hamkuona aibu kudanganya nchi haikopi kumbe inakopa, ndiyo muone aibu bungeni?
Hamkuona aibu kuiba hela za Tegeta Escrow ndiyo muone aibu bungeni!?
Hamkuona aibu trilioni 1.5 za serikali kutojulikana zilikoenda, ndiyo muone aibu Bungeni?
Hamkuona aibu kusema hakuna CORONA Tanzania ndiyo muone aibu Bungeni?
Nyie watu uso zenu ziliumbwa na haya lakini matendo yenu yamewafanya msiwe na haya hata kidogo.
Mtu anayedhani iko siku mtakuja kuona aibu kwa mambo mnayoyafanya, anajidanganya sana.