Uchaguzi 2020 Wabunge wa CHADEMA waliokataa kununuliwa wana nafasi kubwa sana ya kuchaguliwa tena na hii ni ishara ya anguko la wale waliouza utu wao

Uchaguzi 2020 Wabunge wa CHADEMA waliokataa kununuliwa wana nafasi kubwa sana ya kuchaguliwa tena na hii ni ishara ya anguko la wale waliouza utu wao

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Kwa mtazama wangu, matokeo ya kura za maoni ya watia nia wa CHADEMA, yanadhihirisha jambo moja kubwa: Wabunge waliokataa kuuza utu wao, wameaminika sana kwa wananchi na hivyo wana nafasi kubwa sana ya kushinda katika uchaguzi kama walivyoshinda katika kura za maoni.

Mfano ni matokeo haya ya John Heche katika Jimbo la Tarime vijijni:

MATOKEO YA KURA ZA MAONI JIMBO LA TARIME VIJIJINI MGOMBEA ALIKUWA MMOJA AMBAE NI JOHN HECHE

IDADI YA KURA ZILIZOPIGWA: 270

KURA ZA NDIYO: 268

KURA ZA HAPANA: 0

KURA ZILIZOHARIBIKA :02

HIVYO JOHN HECHE NI MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA TARIME VIJIJINI MWAKA 2020 kupitia CHADEMA

Source: Martin M. M on twitter

Ukiacha John Heche, hata Easter Bulaya na Catherine Ruge nao wamshinda kwa asilimia zaidi ya 90 hivyo hiki ni kielelezo tosha kuwa wananchi wamewaamini kutokana na misimamo yao ya kutosaliti wapiga kura.

Wale waliokubali kurubuniwa, wajiandae kisaikolojia kukataliwa maana hata huko walikohama hawatakiwi na walikohama ndio kabisa, sasa sijui watashinda vipi labda kwa kutangazwa washindi jambo ambalo huenda safari hii likakumbana na upinzani mkali sana.

Mambo yakiwa tight katika Majimbo na kata nyini za uchaguzi wakati wa kutangaza matokeo,inaweza kuwawia vigumu wanaotaka kupindua meza ukizingatia pia na ukubwa wa nchi; hivyo, hali inaweza kuwa tofauti na matarajio yao huku Bwana yule nae anaweza kusalimu amri kwa kuacha alieshinda atangazwe mshindi iwapo wananchi watasimama kidete kulinda kura zao.

Jambo lingine ni kuwa, Bwana yule mwenyewe akipata upinzani mkali,muda mwingi atautumia kufuatilia matokeo yake, kwahiyo hatakuwa na muda wa kuwabeba walioshindwa wakati yeye mwenyewe akiwa katika hali tete kwahiyo anaweza kulazimika kuacha kila mtu apambane hali yake.

Hii picha hapa chini ni John Heche akibebwa na wapiga kura wake baada ya kutangazwa mshindi wa kura za maoni:

1594695850052.png
 
Nchi zetu hizi zinahitaji maombi. Unafikiri ni kwanini hawataki uwepo wa tume huru ya uchaguzi? Angalia jinsi vyombo vya ulinzi na usalama vilivyoaminishwa kuwa nchi hii ni ya chama kimoja. Ubabe mwingi kwenye kuikandamiza demokrasia, nk
 
Nchi zetu hizi zinahitaji maombi. Unafikiri ni kwanini hawataki uwepo wa tume huru ya uchaguzi? Angalia jinsi vyombo vya ulinzi na usalama vilivyoaminishwa kuwa nchi hii ni ya chama kimoja. Ubabe mwingi kwenye kuikandamiza demokrasia, nk
Watu wameshaanza kuipuuza tume ya uchaguzi jambo ambalo ni baya, ubabe una mwisho tena mwisho mbaya. Nguvu ya umma ikiamua kuchukua nafasi yake tume haitafua dafu lazima aliyeshinda atatangazwa.
 
Hata ukiangalia tabasamu la vijana wasaliti ni la hofu na aibu. Kule kwa wahaya Bukoba kuna usemi mwanaume anageuka kitandani sio kauli au msimamo, vinginevyo sifa ya kuwa mwanaume inaondoka. Hawa sio wanaume tena.

iamlyenda___CCh5OJRgaQI___.jpg
 
Hata ukiangalia tabasamu la vijana wasaliti ni la hofu na aibu. Kule kwa wahaya Bukoba kuna usemi mwanaume anageuka kitandani sio kauli au msimamo, vinginevyo sifa ya kuwa mwanaume inaondoka.

Hawa sio wanaume tena.View attachment 1506088
Wanaishi kwa aibu sana hawa watu na sijui kama wako comfortable kujichanganya na raia katika majimbo yao.
 
Sasa mbona Erythrocyte kapigwa chini wakati ahuyu jamaa nimpambanaji wa kweli
Demokrasia ndani ya Chadema ni kubwa kuliko mnavyofikiri. Na wanachama sio lazima wakupe ridhaa ya ubunge pekee, wanaweza kuona unafaa zaidi katika huduma nyingine kwa chama zaidi ya ubunge. Wanaomkumbuka marehemu mzee Kimesera watanielewa naongelea nini.
 
Demokrasia ndani ya Chadema ni kubwa kuliko mnavyofikiri. Na wanachama sio lazima wakupe ridhaa ya ubunge pekee, wanaweza kuona unafaa zaidi katika huduma nyingine kwa chama zaidi ya ubunge. Wanaomkumbuka marehemu mzee Kimesera watanielewa naongelea nini.
Yote hii mnahangaika kwa lengo la kutaka kumpora Agnes Lambert ugombea ubunge Segerea aliyemshinda John MREMA kura za maoni ili mumpe John MREMA mchaga mwenzenu ugombea ubunge Segerea kupitia Chadema.

Hizo nia zenu ovu tunazifuatilia
 
Yote hii mnahangaika kwa lengo la kutaka kumpora Agnes Lambert ugombea ubunge Segerea aliyemshinda John MREMA kura za maoni ili mumpe John MREMA mchaga mwenzenu ugombea ubunge Segerea kupitia Chadema

Hizo nia zenu ovu tunazifuatilia
Unadhani ya Magufuli aliyomfanyia Membe yapo ndani ya Chadema?
 
Hata ukiangalia tabasamu la vijana wasaliti ni la hofu na aibu.
Kule kwa wahaya Bukoba kuna usemi mwanaume anageuka kitandani sio kauli au msimamo, vinginevyo sifa ya kuwa mwanaume inaondoka.
Hawa sio wanaume tena.View attachment 1506088
Haa haa siasa ni fursa kwa watu,tuvumilianae tuu.Maana kuna waliohama CCM kwenda Chadema,mkawapokea na kuwafurahia kama Ester Bulaya naa wengine.Hata hawa kuhama ni haki yao kama wanaona huko wanakokwenda wanaona kuna nafasi labda kuliko CDM kuwaposti posti mnawaongezea umaarufu na inaonekana mnaumiaa. Ndio demokrasia hiyooo.
 
Yote hii mnahangaika kwa lengo la kutaka kumpora Agnes Lambert ugombea ubunge Segerea aliyemshinda John MREMA kura za maoni ili mumpe John MREMA mchaga mwenzenu ugombea ubunge Segerea kupitia Chadema

Hizo nia zenu ovu tunazifuatilia
Tuone kwenye hili kama kweli hiyo demokrasia inayosemwa ipo Chadema.Bora umeiweka humu kwenye jukwaaa.
 
Haa haa siasa ni fursa kwa watu,tuvumilianae tuu.Maana kuna waliohama CCM kwenda Chadema,mkawapokea na kuwafurahia kama Ester Bulaya naa wengine.Hata hawa kuhama ni haki yao kama wanaona huko wanakokwenda wanaona kuna nafasi labda kuliko CDM kuwaposti posti mnawaongezea umaarufu na inaonekana mnaumiaa.Ndio demokrasia hiyooo
Kuna tofauti kubwa mkuu. Tunaamini kuwa wajibu wa mbunge ni kuwakilisha na kuwapigania wananchi dhidi ya ukandamizaji. Jee kujiunga chama tawala ni kuwapigania wananchi?

Ni demokrasia kweli lakini picha inaonekana. Hata katika mambo ya dunia Mungu katupa demokrasia ya kuchagua upande. Lakini Kahaba/mchawi anapoamua kuwa Shehe/mchungaji ataitwa ameokoka. Ni tofauti sana na Shehe/mchungaji anapoamua kuwa kahaba/mchawi huyu ataitwa amepotoka na kuharibikiwa na sio mfano bora katika jamii
 
Back
Top Bottom