Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Kwa mtazama wangu, matokeo ya kura za maoni ya watia nia wa CHADEMA, yanadhihirisha jambo moja kubwa: Wabunge waliokataa kuuza utu wao, wameaminika sana kwa wananchi na hivyo wana nafasi kubwa sana ya kushinda katika uchaguzi kama walivyoshinda katika kura za maoni.
Mfano ni matokeo haya ya John Heche katika Jimbo la Tarime vijijni:
MATOKEO YA KURA ZA MAONI JIMBO LA TARIME VIJIJINI MGOMBEA ALIKUWA MMOJA AMBAE NI JOHN HECHE
IDADI YA KURA ZILIZOPIGWA: 270
KURA ZA NDIYO: 268
KURA ZA HAPANA: 0
KURA ZILIZOHARIBIKA :02
HIVYO JOHN HECHE NI MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA TARIME VIJIJINI MWAKA 2020 kupitia CHADEMA
Source: Martin M. M on twitter
Ukiacha John Heche, hata Easter Bulaya na Catherine Ruge nao wamshinda kwa asilimia zaidi ya 90 hivyo hiki ni kielelezo tosha kuwa wananchi wamewaamini kutokana na misimamo yao ya kutosaliti wapiga kura.
Wale waliokubali kurubuniwa, wajiandae kisaikolojia kukataliwa maana hata huko walikohama hawatakiwi na walikohama ndio kabisa, sasa sijui watashinda vipi labda kwa kutangazwa washindi jambo ambalo huenda safari hii likakumbana na upinzani mkali sana.
Mambo yakiwa tight katika Majimbo na kata nyini za uchaguzi wakati wa kutangaza matokeo,inaweza kuwawia vigumu wanaotaka kupindua meza ukizingatia pia na ukubwa wa nchi; hivyo, hali inaweza kuwa tofauti na matarajio yao huku Bwana yule nae anaweza kusalimu amri kwa kuacha alieshinda atangazwe mshindi iwapo wananchi watasimama kidete kulinda kura zao.
Jambo lingine ni kuwa, Bwana yule mwenyewe akipata upinzani mkali,muda mwingi atautumia kufuatilia matokeo yake, kwahiyo hatakuwa na muda wa kuwabeba walioshindwa wakati yeye mwenyewe akiwa katika hali tete kwahiyo anaweza kulazimika kuacha kila mtu apambane hali yake.
Hii picha hapa chini ni John Heche akibebwa na wapiga kura wake baada ya kutangazwa mshindi wa kura za maoni: