Pendekezo la namna hii lilipelekwa ktk bunge la katiba 2014 lakini halikufua dafu, likafeli, na waliolifelisha ni hao hao wabunge ambao asilimia kubwa ndio waliounda bunge la katiba!!
Ila kiukweli ni aibu sana kwa Taifa letu kwa miaka hii kuwa na wawakilishi bungeni level ya std7 au form4
Ila na sisi wasomi tusiishie kulalamika humu mitandaoni, mwaka ndio huu tukachukue fomu tugombee,, Vilaza kama Kina Steve Nyerere, Harmonize, Wema wanapata ujasiri kwenda front kutangaza nia na usishangae baadhi yao wakaokota dodo October,,, wasomi tunakwama wapi!????
Au ndio tusubiri miujiza ya hao Vilaza eti wakaingie bungeni afu tutegemee wapitishe sheria ya 'kujichinja' ya mgombea Ubunge awe with minimal level of degree or diploma or equivalent..!????