Wabunge wa Kenya wamfagilia Magufuli

Wabunge wa Kenya wamfagilia Magufuli

elivina shambuni

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2018
Posts
461
Reaction score
295
1573843242259.png

WABUNGE wa Kenya wamemfagilia Rais John Magufuli, kutokana na kusimamia vizuri mapato na matumizi na ujenzi wa miradi, ambayo thamani ya fedha inaonekana katika utekelezaji wake nchini.

Wakizungumza katika ziara nchini ya kujifunza namna Mfuko wa Jimbo unavyofanya kazi na kutembelea miradi mbalimbali jijini Dodoma, walisema Rais Magufuli ameonesha umahiri wa hali ya juu katika kazi yake, hasa ya kusimamia fedha za umma katika miraadi.

Mbunge wa Turbo na Embakasi Central, Janet Sitienei alisema wao kama wabunge wa Kenya, wanasifu utendaji wa Rais Magufuli na wanapongeza kutokana kwa kusimamia fedha za umma katika miradi na matokeo yake yanaonekana, kwani hakuna senti inayopotea. “Asante Rais Magufuli kwa kazi na thamani ya fedha inaonekana na zinatumika katika kuendesha miradi na kila fedha inatumika vizuri,” alisema Sitienei.

Alisema miradi mikubwa kama ya reli, barabara na viwanja vya ndege, inatekelezwa kwa kusimamia fedha kutokana na usimamizi wa kiongozi huyo. Sitienei alimpongeza Raisi Magufuli, kwa umahiri wa kusimamia miradi mikubwa ya kitaifa, inayotekelezwa katika maeneo mbalimbali jijini Dodoma, ikiwemo ya kuunganisha usafiri Dodoma kwa Reli, barabara, stendi, soko hadi uwanja wa ndege Msalato.

Alisema fedha zilizotolewa kwa ajili ya kujenga stendi ya mabasi zaidi ya Sh bilioni 41 na soko pamoja na ujenzi wa eneo la kupumzikia Chinangali, ni fedha nyingi, ambazo bila usimamizi mzuri wa miradi na thamani ya fedha isingeonekana. Mbunge wa Jimbo la Embakasi Nairobi, Getrudi Mwangi alisema mwanzo alikuwa haielewi vizuri, lakini sasa baada ya kutembelea miradi mikubwa Jijini Dodoma, anaamini jiji hilo litakuwa miongoni mwa majiji bora Afrika.

Mwangi alisema anaeleza hilo kutokana na mipango mingi yenye kuendeleza jiji la Dodoma ambao ni makao makuu ya nchi katika kujenga miundombinu ya barabara, reli, stendi na kuunganisha kwa barabara na reli za ndani hadi uwanja wa Ndege.

Alisema miradi hiyo inaipa sifa Dodoma kama makao makuu ya nchi, lakini pia mpango wake wa miundombinu unaionesha ni jiji lililojengwa katika Karne ya 21, hivyo kinachotakiwa ni kuhakikisha usimamizi hadi miradi inakamilika ni jambo muhimu.

Mbunge Elgon, Fred Kapondi alisema wamefurahi kusikia kwamba ramani ya Mpango Mkakati wa Mji wa Abuja, ilichukuliwa kutoka Dodoma, hivyo Abuja ni mtoto wa Dodoma na kwamba Nigeria inatakiwa kukubali kwamba imejenga jiji hilo kutokana na msaada wa jiji la Dodoma.

linalojengwa katika Karne ya 21, linakuwa bora zaidi barani Afrika. Meya wa Jiji la Dodoma, Prof Davis Mwamfupe alisifu ujio wa Wabunge hao kutoka Kenya na kutembelea ofisini kwake. Alisema wamepokea ushauri kutoka kwa wabunge hao, kwamba ili miradi hiyo iwe endelevu wanatakiwa kuwa na mfumo bora wa usimamizi bora wa miradi hiyo mikubwa kitaifa na makao makuu ya nchi.

Awali, Mkurgenzi wa Jiji Godwin Kunambi alisema Jiji la Dodoma lilipokea kutoka serikali Sh bilioni 77 na sasa baadaye serikali iliongeza Sh bilioni tisa ambazo zinatumika katika kujenga miundombinu mbalimbali, ikiwemo soko, stendi na uwanja wa Msalato na itaunganishwa kwa barabara na reli
 
Mtu anayesifiwa kuwa anatumia pesa za uma vizuri harafu wakati huo hataki ripoti ya CAG iwekwe wazi . ni kujitekenya huko
Kwa miaka hii Roho zenu nyeusi sana mtakoma sana wanaotoka nje Wa naona ukweli mlitaka waone kama nyie mliovaa miwani ya miti mtakufa na Roho zenu hizo ndio maana mnashindwa hata kujenga ofisi hata Rangi hampaki mkitaka vikao hotel bili hamjui inalipwa bei gani
 
Ukweli ni kwamba miaka hii michache ya Magufuli nchi inajengwa sana.
Tena naona ni muendelezo wa awamu ya Mzee J.M Kikwete.
Tanzania imeanza kujengwa kwa kasi sana awamu za hawa maraisi wawili.
The BOOM Country!!
 
Ulitegemea hao wabunge waseme tofauti na walichokisema? Hizo ni sifa za marehemu popote husifiwa.
Mkuu tindo pole sana maana sio kwa maumivu kama hayo ya kwako. Kama wanachokisema kipo na kinaonekana hadharani wao wasiseme kwani wakisema yatakuwa ni yale yale ya marehemu kusifiwa!.
 
Tumia akili ya kawaida tu, umealika watu nyumbani kwako kisha ukawakarimu vizuri, kuna namna yoyote watakuambia mapungufu yako zaidi ya kuisifia nyumba yako? Ndio maana nakuambia sikutegemea kauli tofauti na hiyo.
 
Hautegemei kupondwa na watu wa njee, tunao akina nyie ambao hamna kazi nyingine isipokuwa kuponda kila kizuri cha kwenu.
Ulitegemea hao wabunge waseme tofauti na walichokisema? Hizo ni sifa za marehemu popote husifiwa.
 
Basi kama vipi tubadilishane marais ili kama nao wafaidi tunachofaidi.
 
Hautegemei kupondwa na watu wa njee, tunao akina nyie ambao hamna kazi nyingine isipokuwa kuponda kila kizuri cha kwenu.

Kwani kuna shida sie tusiokuwa na kazi nyingine tunaoponda, wakati mko nyie wenye kazi nyingine ya kusifia tu hayo mnayoita mazuri?
 
RAIA wote wa Africa wanamuitaji magufuli awe rais wao

State agent

Ni kweli ila ni wale raia weusi wanaovamia wageni kama ccm hapa nyumbani dhidi ya wapinzani, ila sio wale weupe wanaojitambua.
 
Kama ambavyo watanzania wanamfagilia kenyata
View attachment 1263971

Back
Top Bottom