Wabunge wa Mbeya hatujasikia kelele zenu juu ya barabara zetu mbovu Bungeni

Wabunge wa Mbeya hatujasikia kelele zenu juu ya barabara zetu mbovu Bungeni

Wabunge wetu mlioko Bungeni, Dodoma mnaotoka Mbeya.

Mtajionyesha umahiri wenu toka siku ya kwanza kabisa bungeni, lakini umahiri huo hatuuoni.
Kero kubwa za Mbeya, kwanza ni barabara.

Main road ya Tanzania kwenda Zambia ni mbaya sana, ukiingia Mbeya mjini malori ya mixigo mizito inapishana na bajaji.
Barabara inabidi ipanuliwe kuwa 4way two lanes, na service rd.

Barabara ya Katumba-Lwangwa- Mbambo-Masoko-Tukuyu umekuwa wimbo wa kasuku.

Barabara ya Mbalizi Makongolosi hivyo hiyo.

Wabunge wetu mna fanya nini?

Miaka mitano si mingi, nanyi mnatujua wananchi wenu huku mkoani tunavyojua kuwageuka tukiona hamfanyi kitu.
Hili ni angalizo.
Kwani yule dadake Salva Kiir anasemaje? Maana alipochukua Jimbo alikuwa na bwembwe
 
Mbeya hatuna mbunge hata mmoja pale bungeni.

Wameenda kutafuta maslahi yao binafsi.
Kwani mliwachagua? Msiwalazimishe wawatetee wakati kuingia Bungeni wametumia mbinu za Medani.
 
Barabara za Tanroad kama sijakosea sio ishu ya kibunge, ni mipango/ilani ya chama chako cha CCM 'bwana macho kwenye ubondo'...

Mfano hiyo barabara ya TAN - ZAM haswa kipande mbele kidogo tu ya Igawa hadi Mbeya (Nsalagha), nadhani ni moja ya barabara mbovu kupindukia za mkoa hadi mkoa kwa sasa...

Ile barabara ina mashimo shimo, ukiwa waendesha gari ni mwendo wa kudance tu ama kupiga mashimo, ukifika mlima nyoka napo kuna mifereji lami imebonyea bonyea hovyo...
Sijasikia popote hawa wabunge wetu wakiishinikiza serikali kujenga upya TANZAM highway.

Huko kuelekea Chato kuna ma Flyover yanajengwa ziwa Victoria.
 
mbalizi makongolosi nmepita juzi ni lami..ukiwa unaenda mkwajuni nd vumbi
 
Nchi hii haitaisha rushwa na vituko.
Tulia amegawa chakula anakiita futari. Wananchi wakimueleza shida nyuma ya kamera hataki kusaidia anataka mpaka wanahabari waiambie dunia.
 
mbalizi makongolosi nmepita juzi ni lami..ukiwa unaenda mkwajuni nd vumbi
Hujui barabara ya kwenda Mkwajuni ni muhimu sana?

Pale kuna Hospitali ya Mwambani ambapo ikitokea mgonjwa amezidiwa inabidi akimbizwe mbeya ?
 
Hata barabara ya Tanzam ambayo ni barabara kuu kuanzia Igawa hadi unaingia Mbeya ni mahandaki matupu, karibu tutaanza kufuga kambale hakika inakera sana, akinaSugu na wenzake walikuwa wanakazana kujenga hoteli zao na kudai respect wakati walikuwa hawafanyi lolote bungeni, inabidi wabunge wa mkoa wa Mbeya waamuke sasa.
Ilijengwa vizuri sana mkoani kwetu hapa Iringa. Si unajua CEO wa TANROADS.....
 
Wabunge wetu mlioko Bungeni, Dodoma mnaotoka Mbeya.

Mtajionyesha umahiri wenu toka siku ya kwanza kabisa bungeni, lakini umahiri huo hatuuoni.
Kero kubwa za Mbeya, kwanza ni barabara.

Main road ya Tanzania kwenda Zambia ni mbaya sana, ukiingia Mbeya mjini malori ya mixigo mizito inapishana na bajaji.
Barabara inabidi ipanuliwe kuwa 4way two lanes, na service rd.

Barabara ya Katumba-Lwangwa- Mbambo-Masoko-Tukuyu umekuwa wimbo wa kasuku.

Barabara ya Mbalizi Makongolosi hivyo hiyo.

Wabunge wetu mna fanya nini?

Miaka mitano si mingi, nanyi mnatujua wananchi wenu huku mkoani tunavyojua kuwageuka tukiona hamfanyi kitu.
Hili ni angalizo.
Unafiki wenu utaeaponza.mlisema sugu hafanyi lolote mkaenda kwa Tulia na Sasa mmeanza kulalamika.hatuwaelewi watu wa mbeya
 
Ilijengwa vizuri sana mkoani kwetu hapa Iringa. Si unajua CEO wa TANROADS.....
Ah kweli hapo umenikumbusha hii ya Iringa kwa kweli utadhani uko mtoni, kumbe CEO kafanya mambo ya mtu kwao,lakini angetukumbuka hata sisi majirani zake bana, sisi sote ni walewale teh teh
 
Unafiki wenu utaeaponza.mlisema sugu hafanyi lolote mkaenda kwa Tulia na Sasa mmeanza kulalamika.hatuwaelewi watu wa mbeya
Ndio Sugu na wabunge wenzake waliopita wa mkoa wa Mbeya hawakufanya chochote zaidi ya kufanya biashara zao, mtu kama Sugu na huyu Amon walikuwa na kazi ya kutafuta vibalivya kujengea mahoteli yao tu na hadi wakajenga kwenye vyanzo vya maji vya hao hao watu ambao ndio waliowapeleka mjengoni.
 
Back
Top Bottom