Wabunge wa Mbeya hatujasikia kelele zenu juu ya barabara zetu mbovu Bungeni

Kwani yule dadake Salva Kiir anasemaje? Maana alipochukua Jimbo alikuwa na bwembwe
 
Mbeya hatuna mbunge hata mmoja pale bungeni.

Wameenda kutafuta maslahi yao binafsi.
Kwani mliwachagua? Msiwalazimishe wawatetee wakati kuingia Bungeni wametumia mbinu za Medani.
 
Sijasikia popote hawa wabunge wetu wakiishinikiza serikali kujenga upya TANZAM highway.

Huko kuelekea Chato kuna ma Flyover yanajengwa ziwa Victoria.
 
mbalizi makongolosi nmepita juzi ni lami..ukiwa unaenda mkwajuni nd vumbi
 
Nchi hii haitaisha rushwa na vituko.
Tulia amegawa chakula anakiita futari. Wananchi wakimueleza shida nyuma ya kamera hataki kusaidia anataka mpaka wanahabari waiambie dunia.
 
mbalizi makongolosi nmepita juzi ni lami..ukiwa unaenda mkwajuni nd vumbi
Hujui barabara ya kwenda Mkwajuni ni muhimu sana?

Pale kuna Hospitali ya Mwambani ambapo ikitokea mgonjwa amezidiwa inabidi akimbizwe mbeya ?
 
Ilijengwa vizuri sana mkoani kwetu hapa Iringa. Si unajua CEO wa TANROADS.....
 
Unafiki wenu utaeaponza.mlisema sugu hafanyi lolote mkaenda kwa Tulia na Sasa mmeanza kulalamika.hatuwaelewi watu wa mbeya
 
Ilijengwa vizuri sana mkoani kwetu hapa Iringa. Si unajua CEO wa TANROADS.....
Ah kweli hapo umenikumbusha hii ya Iringa kwa kweli utadhani uko mtoni, kumbe CEO kafanya mambo ya mtu kwao,lakini angetukumbuka hata sisi majirani zake bana, sisi sote ni walewale teh teh
 
Unafiki wenu utaeaponza.mlisema sugu hafanyi lolote mkaenda kwa Tulia na Sasa mmeanza kulalamika.hatuwaelewi watu wa mbeya
Ndio Sugu na wabunge wenzake waliopita wa mkoa wa Mbeya hawakufanya chochote zaidi ya kufanya biashara zao, mtu kama Sugu na huyu Amon walikuwa na kazi ya kutafuta vibalivya kujengea mahoteli yao tu na hadi wakajenga kwenye vyanzo vya maji vya hao hao watu ambao ndio waliowapeleka mjengoni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…