Wabunge wa Tanzania wajue sio kila jambo linalohusu usalama wa nchi ni la kutolewa ufafanuzi kwa wanasiasa

Wabunge wa Tanzania wajue sio kila jambo linalohusu usalama wa nchi ni la kutolewa ufafanuzi kwa wanasiasa

Mawazo ya hovyo kabisa haya!

Yaani watu kama akina Ben Saanane hawajulikani walipo kwa takribani miezi 18 sasa; wewe unataka kuaminisha watu kwamba mambo kama hayo yanatokea kwa ajili ya usalama wa taifa?!

Mwandishi wa Mwananchi nae unaenda mwezi wa 4 sasa with unknown whereabouts; halafu unataka kuaminisha watu kwamba, hayo hayapaswi kuhojiwa kwa ajili ya usalama wa taifa!!

Kwa mfano, unaweza kueleza ni aina ipi ya security threat iliyosabishwa na mtu kama Ben Saanane kwa kuhoji PhD ya Mkuu wa nchi?!

Ikiwa Waandishi wa Habari wanaruhusiwa kwenda hadi uwanja wa vita kuripoti vita; ni hatari ipi ya kiusalama ambayo ingesababishwa na Ripota wa Mwananchi kwa kutaka kufuatilia kilichokuwa kinaendelea Kibiti?!

By the way, kila mmoja anafahamu Magaidi wakubwa kabisa waliokuwa wanahatarisha usalama wa Marekani walikuwa wanakamatwa na kupelekwa Guantanamo!

Unaweza kutueleza hapa hao wahatarishaji wakubwa wa usalama wa Tanzania wamezuiwa gereza lipi kwa miezi yote hii?!

Btw, hivi unafahamu tofauti kati ya kulinda taarifa za siri za kiusalama (classified info) na kuficha maovu yaliyofanywa na watu walio kwenye system?

All in all, yote yana mwisho haya na endeleeni kutetea udhalimu kwavile hayajawakuta!

Na uzuri ni kwamba, majority ya watetezi wa udhalimu unaoendelea wala hampo kwenye inner circle, na kwa maana nyingine; hata nyie hampo salama!!

Ikiwa hata Nape ameshawahi kutolewa bastola hadharani; seuze nyie ambao wengine hata kula yenu ni shida!!

Wengine mkikesha kuangalia filamu na tathimlia za kivita na kijasusi kutoka Hollywood, mnadhani tayari ndo mmeshakuwa wataalamu na wachambuzi wa masuala ya kijeshi na kijasusi!
Huko Marekani magaidi waliokubali kuwa recruited na kutumika kama double agents wa Al Qaeda walifutiwa mashikata na ofisi ya DPP wa Marekani na kuachiwa kwa kazi maalum kwenda nchi kama Jordan na Lebanon kupeleleza viongozi waandamizi wa makundi mengine ya kigaidi. Waliokataa kutoa ushirikiano walipewa mashtaka mengine zaidi kwa maslahi ya kiulinzi ya Marekani.

Ofisi kama hizo za DPP na AG zinafanya kazi kwa ukaribu mkubwa sana na vyombo vingine vya usalama hivyo msiwalaumu wanapotimiza wajibu wao unaoweza kuwakera nyie kama vile kubambikia watu kesi au kunyima dhamana ila ni kwa maslahi ya taifa. Kwa nchi kama Marekani, kuna wakati kunyima watu dhamana (Coercion) ni muhimu ili mtuhumiwa aweze kutoa ushirikiano kwa dola.
 
Umeongea hivyo kwa vile hao 380 wanaodaiwa kupotea sio baba, mama ako na ndugu zako.
Kumbuka kua mnayowafanyia Watanzania ipo siku yatawafika.
Mana saizi mmekamata vyombo vyote vya habari ili uovu wenu usijulikane. Sawa, ila Mungu si dhalimu.
Mfano wabunge wanaowakilisha majimbo mbalimbali ndani ya jiji la Dar wanaweza kuomba kujua "Informers wa Police" wote waliopo ndani ya jiji zima kwa maana wanalipwa kupitia pesa ambazo ni kodi za watanzania.

Je, hii ni sahihi kwa waziri wa mambo ya ndani kutoa majina yao?
 
Cc MALCOM LUMUMBA uzi wenyewe ndiyo huu wamejazana vilaza wa CCM na TISS huku mtu mmoja anatumia ID zaidi ya moja anaulixa swali halafu anajibu kwa ID nyingine
 
Cc MALCOM LUMUMBA uzi wenyewe ndiyo huu wamejazana vilaza wa CCM na TISS huku mtu mmoja anatumia ID zaidi ya moja anaulixa swali halafu anajibu kwa ID nyingine
Mkuu, yaaani nikiona mtu mmoja anamiliki IDs kibao huwa namuona kama chizi ujue?
 
Back
Top Bottom