Wabunge wa UKAWA kususia Bunge la Katiba kulitokana na Ukosefu wa Elimu, ndio sababu sasa wataingia 'darasani' miaka mitatu

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Kwa Kawaida Mtu aliyeelimika na anayejua Katiba ni nini hawezi kususia Mjadala wa Kibunge wa kutengeneza Katiba.

Mtu aliyeelimika ataelewa wazi Ukishapokea posho unaposusia Vikao ni lazima uwarejeshee Walipa kodi Fedha zao vinginevyo wewe ni mwizi unayepaswa kushtakiwa.

Mtu aliyeelimika ataelewa wazi kabisa kwamba Katiba ni maisha hivyo ataipigania kwa Jasho na Damu badala ya Kususa au Kuzira na kumpa Faida adui "Ukisusa siye twala"

Wananchi waelimishwe kwa hiyo miaka 3 ila Wabunge kama akina Babu Tale wakae darasani miaka 7 dadeki 😂

Mungu wa mbinguni awabariki!
 
Ada na ghalama zote watalipa wananchi wanyonge, darasani kwenye somo la uraia Katiba ipo, au mwalimu kafundisha lakini anadhani hajaeleweka?
 
Kwani katiba si kitabu tu? Sasa INA umuhimu gani?

Wakristo wangapi wana Biblia na hawasomi na waislamu wangapi wana msahafu hawasomi.

Hizo pesa ,a katiba tugawane tu kila mtu aambulie, Tanzania inapaswa kutawaliwa kijeshi tu.
 
Wewe nadhani hujui kilichotokea ni Bora unyamaze kimya usubiri hiyo elimu yako ya miaka 3...... Ile tu ya darasa la Saba ulifeli ambayo ni miaka 7 sasa hii ndiyo utaambulia kitu.
 
Inashangaza sana kijana kama wewe unashabikia mambo kama haya. Una amini kwa sababu sasa hivi ni mmoja wao hivyo hata mjukuuu wa mjukuu wako atakuwa mmoja wao. Watu wanaweza kuwa wamesusia kwa sababu kuna vipengele kandamizi vilikuwepo. Haya mambo ni serious I mean Katiba. Sasa hivi watu wanapiga pesa maana katiba haiwabani. nk..
 
Hii wakafundishane matutusa ya Ccm kwa sababu ndio hawajui katiba ya chama chao na ndio sababu huwa hakuna uchaguzi wowote wa kuchaguwa viongozi wa Ccm Taifa.

Niambie ni Mwenyekiti yupi wa Ccm umewahi kushindana na mwanaccm mwenzake kupigiwa kura? Je katiba ya Ccm inakataza hilo? Hapana, sasa matutusa ya Ccm ndio yasiyojuwa katiba wakayafundishe hayo mazuzu wenzao.
 
Kwani katiba si kitabu tu? Sasa INA umuhimu gani?

Wakristo wangapi wana Biblia na hawasomi na waislamu wangapi wana msahafu hawasomi.

Hizo pesa ,a katiba tugawane tu kila mtu aambulie, Tanzania inapaswa kutawaliwa kijeshi tu.
Umesomeka
 
Inashangaza sana kijana kama wewe unashabikia mambo kama haya. Una amini kwa sababu sasa hivi ni mmoja wao hivyo hata mjukuuu wa mjukuu wako atakuwa mmoja wao. Watu wanaweza kuwa wamesusia kwa sababu kuna vipengele kandamizi vilikuwepo. Haya mambo ni serious I mean Katiba. Sasa hivi watu wanapiga pesa maana katiba haiwabani. nk..
Andiko lake ni la kubeza tu! Ujumbe ameufikisha kwa mtindo mwingine
 
Ungetaja sababu zilizofanya Chadema wasusie bunge la katiba kwa wakati ule, ungekuwa umeutendea haki uzi wako...
 
Kweli kabisa Chadema wanapaswa kupewa Elimu kwanza kabla ya kuanza mchakato wenyewe, maana pasipo Elimu wataanza kuruka ruka tena na kuleta utoto wao tena.
 
Kwa Kawaida Mtu aliyeelimika na anayejua Katiba ni nini hawezi kususia Mjadala wa Kibunge wa kutengeneza Katiba.

Mtu aliyeelimika ataelewa wazi Ukishapokea posho unaposusia Vikao ni lazima uwarejeshee Walipa kodi Fedha zao vinginevyo wewe ni mwizi unayepaswa kushtakiwa.

Mtu aliyeelimika ataelewa wazi kabisa kwamba Katiba ni maisha hivyo ataipigania kwa Jasho na Damu badala ya Kususa au Kuzira na kumpa Faida adui "Ukisusa siye twala"

Wananchi waelimishwe kwa hiyo miaka 3 ila Wabunge kama akina Babu Tale wakae darasani miaka 7 dadeki 😂

Mungu wa mbinguni awabariki!
Dk tale!?
 
Aliyempa mama Abdul ushauri huu amemuingiza chaka kubwa. Nakumbuka yeye mwenyewe aliwahi kusema kuwa kuna kiongozi mmoja wa mstaafu wa CCM aliwahi kumwambia kuwa adui yake siyo wapinzani bali ni yule mwenye shati la kijani mwenzake. Sasa hao hao anaowaamini ndiyo wamempa ajali hii ya kisiasa.
 
Back
Top Bottom