Kwamba na usomi wao wote wabunge walikurupuka tu hawa kutoa taarifa yoyote, sidhani, msimtete huyo jamaa ni jeuli, na anajua jeuli anaitoa wapi. Wanapo kuja wanakuja mikona nyuma wakishapewa wanagalambuka wanakuwa si waungwana tena. Ndiya maana Mgabe aliwatimua kwa ajili ya mambo kama haya haya.
Hapana ndugu tusiwe wa shamba na mambo ya watu,kwa kufuata jazba ,jambo la muhimu si kwenda kujidai mnataka kuchunguza au kutazama kinachoendelea ,hivi tuwaulize hao wabunge kama ifuatavyo :-
i) Walitaka kwenda huko kwa misingi gani ?
ii) Hiyo hoteli haikushuka hapo kama nyota iliyoanguka ,walikuwa wapi ,kama unakumbuka Muungwana alihoji juzi ,mnakuwa wapi wakati watu wanaaza kufyeka ,kuchimba msingi na kuezeka mpaka wanafikia kuhamia,ndio mnakurupuka kutaka kuwavunjia majumba eti hawakufuata sheria ? Muungwana alilenga mbaali sana ,hivyo kaeni chonjo saa mbaya.
iii) Kama mnaona uwekezaji huwo ulikuwa na mizengwe basi wabunge sio kazi yao kwenda huko hotelini kutaka kuchunguza kinachoendelea ,hivi wameona wapi mfumo wa aina hii ?
iv) Labda kwa lugha ya sasa wameona kuna rushwa imetendeka (katika biashara za mabilioni kipo kiwango fulani anapewa anaeifanikisha dili ) ,hata hivyo wabunge hao kama wangetaka kujua njia zilizotumika kumpata muekazaji huyo na ni namna gani alifanikiwa na kuruhusiwa kupewa eneo ambalo ni mali ya asili basi wakukamatwa ukosi ili aeleze stori yote hiyo ni Waziri husika ,Je wabunge wamewahi kuhoji ?
v ) Unajua Maraisi mawaziri huwa wanasafiri nchi za nje na balozi zetu nazo ziko nje zikituwakilisha, sasa kuna watu ambao huwa wanabuni namna ya kuekeza fedha aliyokuwa nayo ,watu wetu hawa viongozi akiwemo raisi wanaposafiri nchi za nje hupata nafasi ya kuzungumza na watu waliojaaliwa kuwa na vijisenti ,hapo huwa wanabadilishana mawazo na wenye vijisenti hivyo hupata nafasi ya kuwakilisha mbinu au njia ambazo anahisi zitazidi kumpatia vijisenti na moja ni hiyo ya kuulizia au kuwakilisha kitu ambazo angependa kuekeza kwa hao viongozi wetu ,aidha mtu anaweza kumwita pembeni kiongozi au kumualika ili ampe mawazo yake kwa kuogopa kuzitoa mbele ya wengine kunawaweza kuhatarisha mpango wake huo na kunyakuliwa na walio mzidi nguvu.
Nchi yetuimeruhusu uwekezaji ,na jamaa amejaribu kuulizia kama ataweza kuekeza katika mbuga za wanyama ,bila ya shaka amejibiwa inawezekana ,kilichofuata ni dili ya mapato ambayo Tanzania kama ni mhusika mkuu au mwenye kumiliki sehemu hiyo atafadika vipi ? hapo ndio penye mchezo ambao muekezaji yeye haumhusu zaidi ya kukubali au kukataa mapendekezo aliyoletewa na Serikali ,kumbukeni hii au hizi sio hesabu za tenda kama ile ya umeme ,hapa ni mtu ambae alisecure uwekezaji katika mbuga na kutaka eneo la mraba kwa kiasi fulani cha mitamraba au mstatili.
Sasa tukirudi kwenye mahesabu ndio serikali iwajibike(Waziri) kulieleza bunge mahesabu hayo yalifikiwa vipi ukilinganisha na mahoteli ya kitalii yaliyomo ndani ya mbuga hizo ,kwa ufupi makisio na muda wa ukodishwaji ,je serikali itakuwa share holder ,au watalipwa kwa ujazo wa asilimia fulani.
La muhimu hesabu hizi zitakuwa zikipitiwa kila baada ya miaka mingapi ,pia siku hizi kuna aina ya ukodishaji ambao unamkodisha mtu kwa miaka kama 50 au mia na akimaliza ,anahama au mnapnga na kuingia nae mkataba upya.
Wabunge hamjakuwa na sababu kuzuka huko na makoti yenu ,haya mambo yanaenda kisheria tena kama mlikuwa makini zipo sheria za kimataifa ambazo zinajulikana kwenye vifungu vya UN. Kilichotokea Zimbabwe huwezi kulinganisha na hapa unaweza kulinganisha na Zanzibar ambako baada ya Mapinduzi waligawana mashamba na majumba yaliokuwa yakimilikiwa na waarabu au watu wakaribu yao ,mbona mashamba yamewashinda na majumba yanaporomoka kila ufikapo msimu wa mvua.
Hivyo kila jambo na mipango yake ,unaweza kusema mnyamwezi anaweza kulima ekari nyingi tu za shamba na akazitunza vizuri na akafanikiwa kuvuna mazao na kuuza na kujipatia fedha lakini huwezi kwenda kumchukua mtu wa pwani kwenye ufukwe ukampa ekari kama za mnyamwezi .ni kupoteza wakati na mnyamwezi huwezi kumpa mtumbwi ukamuambia aende baharini kuvua arudi na samaki .Na ndio mambo yanavyokwenda usione dobi anapata fedha kwa kukusanya nguo za watu na kuwanyooshea ukaona na wewe kazi hiyo unaiweza .wandugu mtakatika mikono na nguo haijapigika pasi pengine ukimaliza shati tu umechoka maji unaita mee.
Sasa mtu anaposema hataki kiwingi katika shughuli zake basi mumfahamu ,pengine ameahidi sehemu hiyo haitembelewi na watu wasio kuwa watalii ,na pengine sehemu hizo zinakuwa half nude wenyewe wanapunga upepo mnawazukia na mabuti na kugongesha viatu kwenye sakafu ,kuweni wastaarabu ,kama mna wasiwasi basi kamataneni mashati huko huko bungeni .
Mna vijisenti wekeni booking mkapumzike ,harudishwi mtu ,labda mnaweza kudai kwa raia kuwepo na kajipasentage fulani kanaondolewa ili wazawa nao wasitoke denda ,hayo ndio mambo ya kuyaomba na sio kuyadai ,mnaomba kwa maneno mazuri na kutongoza mpaka muekezaji anakubali ,sio mnaingia kijeshi ,mambo hayo sasa yamepitwa na wakati ,kuna watu wanatamani wawekezaji wa aina hiyo waende nchini kwao ,Hebu angalieni Botswana , South Africa nafikiri na Namibia wapo wawekezaji wa aina hiyo ,msione kuwa limefanyika hapa Tanzania mkaona ni jambo jipya.
Vipi nchi itaweza kufaidika na hifadhi hiyo ambayo bila ya shaka itakuwa na huduma za kisasa kiasi cha kuitangaza Tanzania na kuwa Holiday destination ,wageni watakaofika sio kuwa watafika hapo tu na kuwa basi ,watatamani kutembezwa sehemu za miji ya wakaazi na humo watakuwa wakinunua bidhaa za wenyeji hao kama kumbukumbu ,na pia wageni watakuwa wakitumia Airport za Nchi na hivyo kuweza kuingiza fedha ya kigeni ,kinachotakiwa ni kujenga infrastructure nzuri ya barabara na viwanja vya ndege ,muwekezaji anaweza kubanwa asianzishe usafiri wa ndege ,ila panaweza kujengwa kiwanja cha ndege ndogo ndogo ambazo zitaweza kutoa huduma za uhakika kati ya sehemu hizo na viwanja vya ndege vya kimataifa .
Na kwa vile wapo wazalendo wanaomiliki ndege na mambo yakikua na wengine wenye vijisenti watajitokeza kuanzisha safari za ndege na mabasi ya kitalii ya kissa kabisa.
Wabunge mnatakiwa kudai katiba mpya ili kuidhibiti nchi na viongozi wake au na serikali yake. Huyo mwekezaji hana hata habari kama mnaibiana wakati alishamwaga saini na serikali yenu.mkimletea fujo atahama tu aende kwengine awaache na mashamba na majumba kama kule zenji sasa wanayia mifuko ya nayloni na imeshakuwa shida wanafinga kwenye magazeti nayo yameshaana kuwa hayapaitikani.
Tunahitaji uongozi safi na katiba mpya sio kuzukia miradi ya watu mkidai mnaenda kuchunguza si bora kwanza muichunguze serikali yenu na halafu mkimaliza huko mtakuwa mmekwisha jua kila kitu mnakaa na wawekazi mnahadithiana na mambo yanasawazishwa ,halafu na hao viruka njia wanaojipeleka na kukatiza kwenye sehemu zilizotiliana saini na serikali mnastahili kupigwa risasi ,mnakwenda kufanya nini huko kama si kuiba mali ya serikali au mnakwenda kupiga chabo ?