Mkuu! Kwa nini usiturahisishie na kutueleza tu kuwa hiyo sheria inasema nini kwa kifupi? Kama hiyo sheria inawaruhusu hao waheshimiwa kuingia popote watakapo kwa kisingizio kuwa wanafuatilia mambo, itakuwa kazi! Kwa nini hatukuwasikia Mikumi Wildlife Lodge, Savoy Hotel Morogoro, KNCU Hotel, Tabora Railway Hotel, Kigoma Railway Hotel, Musoma Railway Hotel, Mafia Wildlife Lodge, Kilimanjaro Hotel wakati zikiwa katika matatizo? Leo imekuwa nongwa kwa sababu ni mgeni anayehusika? Kwenye hoteli aliyojenga kwa pesa zake na si mkopo wa serikali yetu? Halafu tunaandaa tamasha kubwa kuwakaribisha hao hao waje kuwekeza nchini mwetu wakati wale waliokuweko hatuwapi heshima wanayostahili! Maji tumeyavulia nguo, inabidi tuyaoge. Huu ni mfumo tuliouchagua na haki ya mtu binafsi ni mwiko mkubwa! Kama hiyo sheria unayoizungumzia, Mkuu, inawapa haki hawa jamaa kuwa demi-gods, basi hii nchi inaelekea kubaya!