BANDOKITITA
JF-Expert Member
- Oct 4, 2022
- 1,484
- 2,852
Kuna kitu hakiko sawa katika ajira za Tanzania hasa kwenye upande wa ajira za majeshi.
Hivi walioweka kigezo cha mtu ili apate nafasi ya Uhamiaji, JWTZ, Police, Magereza, na Fire eti lazima awe amepitia JKT waliwaza nini na kwa manufaa ya nani?
Kama tujuavyo siyo kila mtu au mhitimu yeyote anaweza kupata nafasi ya kujiunga na JKT. Mfano, siyo wahitimu wote wanao hitimu kidato cha VI huchaguliwa kujiunga na JKT kwa mjibu wa sheria. Hata wale wahitimu wa darasa la VII na kidato cha IV siyo wote wanaojiunga na JKT kwa hiari.
Sasa inakuwaje kigezo hiki kinatumika kama namba 2 baada ya umri kama kigezo muhimu kuliko vyote. Je, hii Iko sawa? Ni nani aliepitisha huu utaratibu.
Kigezo hiki kimekuwa chanzo cha vijana wengi kushindwa kutimiza ndoto zao katika kulitumikia Taifa lao upande wa majeshi kwani kimekuwa kigezo cha moto kwelikweli. Walileta kigezo cha maumbile (urefu wa kimo flani) pasipo kuzingatia mazingira na asili ya Watanzania lakini wananchi wakazoea. Ila sasa hiki kigezo cha JKT kimekuwa msumari mwingine wa moto kwa vijana.
Ni kweli inawezekana niia na shabaha ya vijana kujiunga na JKT km sehemu ya kudumisha uzalendo vilikuwa na mashiko. Tatizo limeonekana pale ambapo jambo hili kuwa kigezo cha msingi katika kujiunga na Majeshi ya Ulinzi na Usalama. Kwa kweli suala hili linatakiwa kupigiwa kelele na wazazi wote pamoja na Wabunge ambao ndiyo wawakislishi na watunga sheria kwa niaba ya wananchi.
Kama kigezo hiki hakitaondolewa au kufanyiwa marekebisho, basi tutegemee kuona upendeleo wa waziwazi na kukithiri kwa rushwa katika ajira hizi za majeshi. Hakuna sababu zozote za kisayansi zinazooonesha kuwa mtu akipita JKT ndiyo anakuwa mzalendo.
Swali ni je, hawa wote wanaokwarapua pesa za walipa Kodi na kuripotiwa na CAG kila mwaka wao wote hawakupitia JKT? Kama kupitia JKT ndiyo kigezo cha uzalendo na uungwana kwa mtumishi kwa nini hawa wanaokwarapuwa pesa za umma wasipelekwe huko JKT?
Tusijifiche katika kigezo Cha JKT kwani uzalendo wa mtu kwa Taifa lake umo moyoni kwake na ni kitu ambacho mtu haitaji kufundishwa darasani bali uzalendo ni km imani ambayo mtu anazaliwa nayo, anakuwa nayo, anakufa nayo na kuzikwa nayo. Haitaji kumaliza vidato au madaftari na kalamu madukani ili kufundishwa.
Nimshukuru mbuge mmoja leo akiwa bungeni kakemea vikali hiki kinachoitwa kigezo namba 2 Cha JKT kujiunga katika majeshi ya ulinzi na usalama. It's not fair, it's not fair, it's not fair at all. Let's share the available national cake equally without segregation of any kind.
Nawatakia usikuvu na utekelezaji mwema wahusika wote.