Wabunge wakemee kwa nguvu zote kigezo cha kujiunga na majeshi kwa sharti la kupitia JKT

Nadhani hizo kazi ambazo umelist hapo ni kazi ambazo zinahitaji vijana na mabinti wakakamavu. Namna rahisi ya kuwabaini ni kwa kupata vyeti vya mafunzo ya jkt ili kuwarahisishia kazi ya usaili wasimamizi wa hizi taasisi ulizotaja.

Kuna kazi kubwa sana kwenye kutrain watu wanakuja watu legelege zoezi kidogo wanalialia, wanaanguka, wanapata matatizo ya kiafya, fujo zinakuwa nyingi na hii inawapa usumbufu sana hawa wanaofanya usaili. Unakuta wamejipanga kuchukua labda candidate 2000 wanakuja kuomba watu 5000 wakianza kuwafanyia mchujo unakuta wanabakia na wenye vigezo 400,wengine wote ni rejected hawafai kwa sababu mbali mbali kama madhaifu ya kimwili yaani afya, tabia mbovu, kukosa nidhamu, kimo kisichosahihi na physical defects, kuna hata wengine miaka hii katika ukaguzi wanawabaini kuwa wameingiliwa kinyume na maumbile au wanaingiliwa. Sababu zipo nyingi sana.

Namna rahisi ni kwa wao kurahisishiwa mchujo kwa kuchukua vijana na mabinti ambao wamefuzu na kuhitimu mafunzo ya JKT na hivyo wakiwapokea kazi ya kuwatrain na kuwarecruit inakuwa rahisi sana bila kupoteza muda na rasilimali nyingi zaidi.
 
Nadhani watu hamkuelewa hoja yangu. Sipingi watu kupitia JKT ndiyo maana hapo juu Kuna mtu nimemwambia tangu zamani huko nyuma asilimia kubwa ya wafanyakazi wa umma ilikuwa lazima uhudhurie mafunzo ya JKT kabla ya kuanza ajira yako tena ilikuwa mwaka 1 siyo hivi vya miezi 6. Hoja yangu ni kuwa km kigezo ni JKT basi kila mhitimu apewe nafasi kujiunga. Siyo km ilivyo sasa wachache wanaomaliza form 6 ndiyo huchaguliwa tena pasipo vigezo vya wazi kuitwa kwenda JKT kwa mjibu wa sheria. Group kubwa hubakia na linapokuja suala la ajira kigezo Cha JKT kinawatoa. Sijui km unanielewa.

Hata wale darasa la 7 au Form 4 wanaoenda kujitolea kwa hiari siyo wote hupata nafasi kulingana na uchache na upungufu wa malazi ktk kambi husika. Wengi wao hubakia. Hivyo kigezo Cha JKT ni ngumu kukitekeleza. Hoja ipo hapo siyo kupinga kupitia huko JKT km ambavyo wengi humu wanavyotofasiri mada hii.
 
Back
Top Bottom