Wabunge wana misamaha ya kodi? Jerry Silaa hakusema wabunge hawakatwi PAYE

Wabunge wana misamaha ya kodi? Jerry Silaa hakusema wabunge hawakatwi PAYE

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Binafsi sikushangaa kabisa kumuona Jerry Silaa akiingia na lundo la vitabu na manual zinazoelezea sheria za kodi.

Kinachonishangaza ni baadhi ya wadau kumtaka Jerry Slaa kuiweka hadharani salary slip yake ili tuone namna asivyolipa kodi kana kwamba Jerry alisema wabunge hawakatwi PAYE.

Swali muhimu ni Je wabunge hawana misamaha ya kodi?

Magari wanayokopeshwa wanalipia kodi?

Hotel wanazojenga hamna namna wanapata unafuu kwenye manunuzi ya vifaa vya ujenzi?

Kodi ni suala mtambuka na upigaji uko kwenye " exemptions "

Jumaa kareem!
 
Hii michezo yenu mwishowe huisha kimya kimya huku wananchi wakiendelea kupigika, upuuzi tu, kama hao wabunge hupiga kura kupitisha tozo kwa watanzania wa hali ya chini sioni umuhimu wao, ni wahujumu uchumi tu.
 
Afafanue ni kodi gani hawalipi. Hilo la msamaha wa kodi kwenye magari ni stahili ya watumishi wote wa umma na sio wabunge peke yao. Sidhani kama wanapewa msamaha kwenye vifaa vya ujenzi n.k.

Amandla...
 
Jerry ni msema kweli, wanamsumbua kwa kusema ukweli.
 
Afafanue ni kodi gani hawalipi. Hilo la msamaha wa kodi kwenye magari ni stahili ya watumishi wote wa umma na sio wabunge peke yao. Sidhani kama wanapewa msamaha kwenye vifaa vya ujenzi n.k.

Amandla...
Watumishi wote wa umma wanzpata msamaha wa kodi ya magari?
 
Watumishi wote wa umma wanzpata msamaha wa kodi ya magari?
Ndivyo ilivyokuwa. Lakini walibadilisha ikawa ni serikali ndio inayomlipia kodi hiyo mtumishi wa umma. Kwa hiyo technically msamaha haupo bali serikali inabeba mzigo wa hiyo kodi.

Amandla...
 
Watumishi wote wa umma wanzpata msamaha wa kodi ya magari?
Ukweli ni kwamba Bunge linatumia mbinu kukwepa kulipa kodi halisi ya kipato chao. ni uhalifu sawa na wengine tu. Huwezi kusema mshahara ni milioni 2 halafu posho ni milioni 8. Ni mtindo wa kishenzi na upuuzi wa kimaadili! Tunataka walipe kodi inayolingana na kipato chao, FINITO!

Kama ni hivyo mishahara ishushwe hadi elfu 60 halafu kuwe na posho ya milioni 4.
 
Nimekuelewa bwashee!
 
Ukitaka kupata matatizo nchini Tanzania, we gusa maslahi ya CCM tu hakuna rangi utaacha kuiona,utatengenezewa kesi mbalimbali chini ya uratibu wa police
 
Sasa si ndiyo msamaha wenyewe?
Hapana. Msamaha ni kuwa deni linakuwa halipo. Hapa deni lipo lakini unalipiwa. TRA wataendelea kukudai mpaka litakapo lipwa na serikali. Msamaha ni kuwa TRA hawapati kitu, kama ilivyokuwa kwa taasisi za kidini.

Amandla...
 
Afafanue ni kodi gani hawalipi. Hilo la msamaha wa kodi kwenye magari ni stahili ya watumishi wote wamma na sio wabunge peke yao. Sidhani kama wanapewa msamaha kwenye vifaa vya ujenzi n.k.

Amandla...
ndugu huu uongo wa watumishi kupata msamaha wa kodi kwenye magari umeutoa wapi nakushauri urudishe ulikoitoa kabla haijakuathiri
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Ukweli ni kwamba Bunge linatumia mbinu kukwepa kulipa kodi halisi ya kipato chao. ni uhalifu sawa na wengine tu. Huwezi kusema mshahara ni milioni 2 halafu posho ni milioni 8. Ni mtindo wa kishenzi na upuuzi wa kimaadili! Tunataka walipe kodi inayolingana na kipato chao, FINITO!

Kama ni hivyo mishahara ishushwe hadi elfu 60 halafu kuwe na posho ya milioni 4.
Haswaa! Nafikiri kuna haja baadae kuweka kwenye katiba zuio la wabunge kutunga sheria zinazowapendelea.
 
Back
Top Bottom