Lady Whistledown
JF-Expert Member
- Aug 2, 2021
- 1,183
- 2,100
Wakuu!
Ni jambo la kusikitisha kuona jinsi ambavyo baadhi ya wabunge wetu bado hawajafahamu vizuri majukumu yao ya msingi kama wawakilishi wa wananchi.
Katika kipindi hiki ambacho nchi inapitia changamoto nyingi kama ukosefu wa ajira, mfumuko wa bei, ubovu wa miundombinu, huduma duni za afya, elimu isiyo na tija, na ukosefu wa uwajibikaji serikalini tunaona mbunge anatumia nafasi ya kuuliza swali bungeni kuomba makoti ya baridi kwa askari polisi wa Mbeya.
Swali hili lingeweza kuulizwa na OCD wa Mbeya kwa maandishi, si kutumia dakika za dhahabu za bunge ambazo zilipaswa kujikita katika masuala ya sera, mifumo ya utawala, na changamoto kubwa za wananchi.
Inasikitisha zaidi pale ambapo serikali inajibu kuwa makoti hayo tayari yanatolewa! Hii inaonesha wazi kuwa:
Bunge ni jukwaa la kisera na la kuchochea mabadiliko makubwa ya kifikra, kiuchumi na kijamii. Wabunge hawako pale kupeleka ombi la makoti kana kwamba ni wasaidizi wa idara za serikali, wao wako pale kusimamia uwajibikaji, kuhoji matumizi ya bajeti, kubuni sera bora na kuhakikisha sauti za wananchi waliowachagua zinasikika.
Tunapaswa kujiuliza kwa sauti kubwa: Wabunge wetu wanajua kilichowapeleka bungeni? Au wamekuwa mawakala wa kushughulikia vitu vidogo vidogo kama makoti, badala ya mabadiliko makubwa yanayogusa maisha ya wananchi?
Huu ni mwito kwa wapiga kura: tutumie vizuri haki yetu ya kuchagua. Tuchague watu wenye maono, uelewa na dhamira ya kweli ya kuleta mabadiliko, si watu wanaochanganya Bunge na ofisi ya kata.
…………………
Mbunge wa Viti Maalumu, Suma Fyandom ameiomba Serikali kuwapatia makoti ya kujikinga na baridi kali askari polisi wanaofanya kazi katika Mkoa wa Mbeya
Akijibu hoja hiyo Naibu Waziri wa, Mambo ya Ndani ya Nchi, Daniel Sillo amesema makoti ya kujikinga na baridi kali ni miongoni mwa sare ambazo askari wanaofanya Kazi mkoani Mbeya hupewa. Ameeleza Mikoa mingine inayopewa makoti ya kujikinga na baridi ni Iringa, Njombe, Songwe, Arusha, Rukwa, Manyara, Kilimanjaro, na Tanga
Chanzo: Azam TV

- Mbunge hajafanya utafiti wa kina.
- Mbunge hafahamu hali halisi ya eneo analoliwakilisha.
- Mbunge anatumia jukwaa la Bunge kwa mambo madogo yasiyo na uzito wa kitaifa.