Tulia hebu tulia umsome mdau huyu halafu ubatilishe kauli yako ya kutaka watu wajitolee ili wapate kipaumbele kwenye ajira!! Wewe utampenyeza nduguyo mahali wanapoptoa posho nzuri kwa wanaojitolea halafu apatiwe ajira! Wakati wengine hata fursa ya kujitolea bure katika maana halisi ya bure HAWAPATI, halafu unataka wasipewe kipaumbele kwenye ajira!! Naomba USHINDWE!!
'Nafasi za kujitolea zenyewe ni connection,unapeleka barua kwa mganga mkuu wa Wilaya inapita miezi kila ukienda unaambiwa kikao hakijakaa.
Mimi nilionyeshwa Hadi store ya mafaili yaliyojaa barua za maombi ya kujitolea, kisha nikaambiwa lazima uwe na mtu wa kuiboost barua yako ili isiingie kwenye mafaili ya store,hiyo ilikua mwezi wa kwanza mwaka huu(2023).
Nilitafuta sehem nikalia na Mungu wangu,then nikaenda home. Nilirudi kwa matron wa hospitali niliyo hitaji kujitolea nikamweleza yaliyojiri kuhusu barua, aliishia kuniambia pole sina nachoweza saidia,wenzio pia wanarudi nakuniambia taarifa mbalimbali.
Nilijaribu kurudi February na March kwenye ofisi ya mkurugenzi wa wilaya.
Kuna dada wa masijala akaniambia,"suala la kuvolunteer sio la haraka kiivyo, katibu yupo busy sana, utajulishwa barua yako ikijibiwa, namba za mawasiliano siumeandika kwenye barua?
Tutakutafuta kwa simu."Mpaka leo tar 7 mwezi wa 4,2023 hakuna kitu.
Nimesema sijitolei tena na hapo nilikua naomba kujitolea hospitali ya wilaya ambapo nilikua nimeambiwa na matron wa hospitali hiyo kuwa, wanauwezo wa kuwalipa posho volunteer 15 tu (tsh.150000),hivyo mie nikiongezeka ntakua silipwi chochote, lakin sikujali nikasema acha niihudumie Jamii yangu.Ila kilichonikuta kwenye kutafuta barua,kimenifanya nijiajiri.
1.SUALA LA KUAJIRI WALE WANAOJITOLEA SI SAWA HATA KIDOGO,KWA SABABU NAMNA YA UPATIKANAJI WA HIZO NAFASI ZA KUJITOLEA UMEJAWA NA SINTOFAHAMU.
2.KIJANA AMEHITIMU CHUO 2018,YUPO MTAANI KWA MIAKA MITANO SASA HUENDA ANAFAMILIA YAKE KABISA ,JE AACHE KUJIAJIRI AENDE KUJITOLEA BILA MALIPO?
NOTE: NAISHAURI SERIKALI KUAJIRI VIJANA KUANZIA MIAKA ILE WALIPO SIMAMISHA AJIRA,VIJANA WANAMIAKA ZAIDI YA NANE MTAANI.WAAJIRIWE WALIOMALIZA AWALI YA WENGINE.
3. HOSPITALI ZA WILAYA NA BAADHI ZA MIKOA HAZINA UWEZO WA KULIPA NUSU MSHAHARA VOLUNTEER,JE WOTE TUKAJITOLEE MUHIMBILI SABABU PALE MALIPO MASHALLAH?
KIUHALISIA WATU WANALIPWA MPAKA 80000/=JE SERIKALI INATAMBUA HILI??KWA POSHO HII MWENYE FAMILIA ATAISHIJE??AMA HATAKIWI KUAJIRIWA NA SERIKALI PALE ANAPOSAKA TONGE MTAANI?
MWISHO: NAIOMBA SERIKALI IPUNGUZE PSYCHOLOGICAL TORTURE KWA VIJANA, MNATUPA DEPRESSION, TUMIENI HEKIMA, VIJANA TUNAHITAJI AJIRA NA SISI TUSIOKUWA NA CONNECTION.
TUPO MIKOANI, HOSPITALI ZINAJENGWA TUNAZIONA LAKINI HATUPATI FURSA YA KUIHUDUMIA JAMII YETU. TUMERUDI NYUMBANI KULIMA SABABU HATUNA UWEZO WA KUKAA MIJINI KWENYE MAHOSPITALI YENYE UWEZO WA KULIPA MAVOLUNTEER VIZURI SABABU HATA NAFASI YA KUVOLUNTEER HAIPATIKANI KWA HAKI, NASI TUNAOMBA MTUAJIRI HUKUHUKU VIJIJINI KWETU TUINUFAISHE JAMII. SUALA LA KUJITOLEA NI FUMBO KUBWA, MLITIZAME.
TUNAMIAKA MINGI MTAANI, TUNAHITAJI FAIR OPPORTUNITY KWENYE AJIRA."
Thanks Quote Reply
"