Tunategemea Wabunge wawe watetezi wa wananchi kwenye masuala mbalimbali kurahisisha maisha yetu badala yake wao ndio wamekuwa wawakilishi wa serikali kutugandamiza.
Wabunge wameridhia serikali kupunguza kodi kwenye bia na kuongeza kodi kwenye mafuta ya petrol, hawaoni kuwa ni mzigo kwa mwananchi, wameongeza tozo ya kodi kwenye miamala ya simu, mbaya zaidi wazo hili lilitolewa na mbunge kwa mgongo wa kodi ya uzalendo.
Wabunge ni wabinafsi sana eti mshahara wao hautoshi wanaomba waongezewe, wanajiona wao ni special kuliko madaktari, wanapokea sh 13.8M kwa mwezi mbali na posho ya sh 120,000 ya kikao kwa siku, hii kama sio dharau kwa wananchi nini.
Hawana faida kwetu na kwa nchi wamebaki kututungia sheria mbovu na kandamizi, binafsi sioni faida ya mbunge wangu zaidi ya kujinufaisha yeye na familia yake kupitia kura yangu.
Wanatudharau sana sisi wananchi, hawako ‘accountable’ wala ‘resiponsible’ kwa wapiga kura wao kwa vile wanajua once wakishachaguliwa hakuna wa kuwawajibisha hadi miaka 5 iishe.
Nashauri tuirejee katiba ya Warioba iliyopendekeza wabunge kama hawa tuwaondoe hata kabla ya kipindi chao kwisha, bila kufanya hivyo wataendelea kutuona sisi wapiga kura wajinga siku zote.