Wabunge wataka Condester Sichwale aliyetolewa nje kisa mavazi aombwe radhi

Yule mzee ni msikiti, hivyo alitaka huyo dada avae hijabu ndio aridhike. Ila bunge futuhi nalo lina vituko vyake acha tu.
Ha ha ha!!!! Kweli bunge futuhi hili!!!!
 
Ningekuwa spika...ingawa siwezi kuwa spika...ningeamuru wote wanaoendeleza huu mjadala watoke nje kabisaaaa....hivi hakuna changamoto za wananchi wao majimboni mpaka hili liwe Jambo serious HIVI?

Kwani wametumwa na wananchi au Magufuli ndio aliwaingiza bungeni kwa kunajisi uchaguzi, ili wamuongezee muda wa kukaa madarakani?
 
Mwendazake alijipambanua kama mzalendo, lakini kwa maoni yangu mimi naona hakuwa Mzalendo, ila alikuwa na ajenda yake ambayo alitaka kuipitisha kupitia neno la uzalendo.
Badala kujadili mambo muhimu ya kitaifa, watumishi wanaiba kwa kujilipa posho hadi 300m kwa wiki. Bunge la ccm linajadili mavazi, afu mtu anasema Magufuli (aliewaleta hawa bungeni) ni shujaa

Sent from my vivo 1611 using JamiiForums mobile a
 
Job ndugai ni mwanasiasa aliyebarikiwa nguvu nyingi kuliko akili.
 
Wamempaisha, wengine ambao tulikuwa hatumfahamu tunaanza kumfuatilia
 
Hivi unafahamu Unachokiongea ?!!

Mbunge anashtakiwa vipi kwa kuongea mawazo yake ndani ya bunge ?!!!

Tena mawazo Yake yalipokelewa na kutafsiriwa kikanuni na MKUU WA SHUGHULI ZA BUNGE(mh.Spika).......

Na bahati iliyoje alikuwepo mh.Spika Mwenyewe kwani kinyume chake labda "uamuzi usingekuwa ulivyokuwa"....

#KaziIendelee
 
Wazee wa siku hizi bana asije kuwa aliomba mzigo kanyimwa sasa akabakia na lake moyoni..!!
 
Sisi tulishauri wabunge washonewe uniform kama student wavae sare Ili kuepusha haya awakusikia
 
Job anayejinasibu kuwa mtetezi wa wanawake mbona ameshiriki udhalilishaji huu? au yeye kapewa kazi ya kuwatetea covid-19 pekee!! yetu macho mwaka huu kila jambo linakwenda against huyu jamaa !!
 
Huo ni udhalilishaji huyo mama amejisitiri na mavazi yake hayana shida yoyote
Labda ule mkia wa mbele ndo tatizo.
But tuwajuavyo ccm wakitaka kupitisha yao ni lzm waandae tukio
 
Na spika anatakiwa amuombe msamaha kwani amekosea, huwezi kutoa hukumu kutokana na macho yako, toa makosa yaliyokua kwenye nguo aliyovaa na taja sifa za mavazi ya wanawake ambayo yanaruhusiwa. na Je spika na yule mzee aliyetoa hoja ni wataalamu wa mavazi? kwanini wasiajiri wataalamu kwa ajili ya kuwashauri na wengine kukaa mlangoni kwa ajili ya ukaguzi? usikubali uzalilishaji kwenye chombo kikubwa kama kile, kwani italeta mazara makubwa kwenye jamii, watoto wa kike watazalilishwa kila mahali kwa sababu ya maumbo Yao tu. lazima hawa watu wawajibike kwa uzalilishaji ulitokea kwenye chombo kama kile.
 
Sasa nani awajibike ?!!!

Awajibike kwa nani ?!!

Mh.Spika atolewe uspika kwa jambo hilo ?!!

Mbunge wa Nyang'wale afukuzwe bungeni kwa jambo hilo ?!!

Hayo yote usemayo yana sheria nyuma yake kuyafanikisha ?!!
 
Ningekuwa spika...ingawa siwezi kuwa spika...ningeamuru wote wanaoendeleza huu mjadala watoke nje kabisaaaa....hivi hakuna changamoto za wananchi wao majimboni mpaka hili liwe Jambo serious HIVI?
Hili jambo ni muhimu sana kwani linaleta uzalilishaji kwa watoto wa kike na kuwaweka kwenye hatari, na heshima ya chombo kama kile kama kuna tatitizo wangetumia njia ya staha kumjulisha mhusika, na watoe sababu sio kwa kuangalia na macho tu na kutoa maamuzi. ili kufuta huo uzalilishaji ni lazima waombe msamaha hazarani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…