Wabunge wataka Condester Sichwale aliyetolewa nje kisa mavazi aombwe radhi

Wabunge wataka Condester Sichwale aliyetolewa nje kisa mavazi aombwe radhi

Hata hivyo mbunge Hussein Amar amesema hawezi kuomba radhi kwa sababu alichosema alikuwa sahihi kwakuwa mavazi aliyovaa mbunge mwenzake hayakuwa na staha ndiyo maana Spika wa Bunge Job Ndugai aliridhia hoja aliyoitoa yeye (Amar).
Ndugai anaweza kuridhia bila 'kujitambua au kuelewa alichoridhia' 🤣
 
Sasa nani awajibike ?!!!

Awajibike kwa nani ?!!

Mh.Spika atolewe uspika kwa jambo hilo ?!!

Mbunge wa Nyang'wale afukuzwe bungeni kwa jambo hilo ?!!

Hayo yote usemayo yana sheria nyuma yake kuyafanikisha ?!!
Uzalilishaji ni kosa na sheria zinazosimamia kosa hili zifuatwe kumbuka hakuna aliyejuu ya sheria
 
Uzalilishaji ni kosa na sheria zinazosimamia kosa hili zifuatwe kumbuka hakuna aliyejuu ya sheria
Ni kweli hakuna aliye juu ya sheria....

Hoja yangu ni kuwa ni sheria ipi iliyovunjwa ?!!

Una uhakika mbunge wa Nyang'wale alikusudia Kumdhalilisha mh.Condester ?!!!

Je mh.Spika naye amemdhalilisha mh.Condester?!!

Je hakuna taratibu za uvaaji mule bungeni ?!!!

Hivi unaelewa kuwa hata ukivaa KANZU na KIBARAGHASHIA bila ya KOTI unaweza kutolewa ?!!
Je ukitolewa utakuwa umedhalilishwa ?!!!

Ama unalalamika KIHISIA tu kujustify "HAKI ZA AKINAMAMA" pasina WAJIBU ?!!!

#KaziIendelee
 
Rudia post vizuri unaenda nje ya nilichoandika awali, tunafuata sheria,taratibu na mingozo, Toa makosa ktk nguo alivaa au unamhukumu mtu kutokana na umbo lake?
 
Kama dini yake inamruhusu kuvaa kiuchiuchi angeachwa tu, kwani kuna ajabu gani? Hiyo mbona kawaida sana kwa jamii nyingine/ ingawa serikali haina dini?
 
Rudia post vizuri unaenda nje ya nilichoandika awali, tunafuata sheria,taratibu na mingozo, Toa makosa ktk nguo alivaa au unamhukumu mtu kutokana na umbo lake?
Sawa....

Kamwe siwezi kumhukumu mtu kwa MAVAZI YAKE....

Hivi unadhani bungeni hakuna TARATIBU ZA MAVAZI ?!!!

Kuhusu kuchambua mavazi yake hapana siwezi kwani namheshimu mh.Condester na kazi hiyo ILISHAFANYWA na mh. SPIKA na alijiridhisha....

Suala fikirishi ni kuwa ,ni kwanini SIKU NYINGINE MH.CONDESTER hakunyooshewa KIDOLE?!!!

Unataka kusema kuwa ni mara ya kwanza kwa mh.Mbunge wa Nyang'wale kumuona mh.Condester?!!
 
Naomba namba ya simu ya Mbunge huyu aliyeonewa. Wengine tuna kipaji cha kuliwaza watu!
 
"kuna wabunge wanatamka kiungo Cha Mwanamke na wengine wanafurahi tu" duh.!
 
Yule mzee ni msikiti, hivyo alitaka huyo dada avae hijabu ndio aridhike. Ila bunge futuhi nalo lina vituko vyake acha tu.
Unamaanisha yule mzee ni muislamu?
Hivi wanawake wasiokuwa waislamu hawavai hijabu? Pale bungeni hapakuwa na wanawake wengine ambao hawakuvaa hijabu? Kwanini amseme yule tu
 
Sakata la kutolewa nje kwa mbunge wa Momba, Condester Sichwale (CCM) kuhusu mavazi, limeibuka tena leo jioni katika kikao cha Bunge baada ya wabunge wanawake kutaka aombwe radhi na aliyetoa hoja.

Hata hivyo mbunge Hussein Amar amesema hawezi kuomba radhi kwa sababu alichosema alikuwa sahihi kwakuwa mavazi aliyovaa mbunge mwenzake hayakuwa na staha ndiyo maana Spika wa Bunge Job Ndugai aliridhia hoja aliyoitoa yeye (Amar).

Katika kikao cha leo jioni wabunge Jacqueline Ngonyani na Stella Manyanya waliomba mwongozo wa Spika kwa madai mbunge aliyetolewa nje alionewa.

Mapema leo Sichwale alitolewa nje kwa amri ya Spika baada ya Amar kuomba mwongozo kwa kutumia kanuni 170 kuhusu mavazi ya staha.

Ngonyani amesema kilichotokea ni kwamba mbunge huyo alionewa kwani alikuwa na vazi la staha ambalo halikuwa na shida lakini akasema huenda Spika hakuona.

"Mimi ni mjumbe wa Baraza Kuu la wanawake wa CCM, ninapoona kuna uonevu lazima niseme na hili sikiungi mkono huyu mwanamke mwenzetu ameonewa,"amesema Ngonyani.

Mbunge huyo amesisitiza kuwa uonevu wa namna hiyo haupaswi kuvumiliwa kwakuwa umemdhalilisha mbunge huyo na wapiga kura wake jimboni.

Kwa upande wake Manyanya amesema tangu asubuhi alikuwa anafuatilia kwenye mitandao na amebaini kuwa Sichwale hakuwa na vazi baya.

Hata hivyo Manyanya amesema haiwezekani wabunge vijana wavae mavazi kama wanayovaa wabunge wanawake watu wazima.

Amesema katika siku za karibuni limeibuka suala la kutoa lugha za kuwadhalilisha wabunge wanawake ndani ya ukumbi ambako wakati mwingine hutamkwa kiungo cha mwanamke halafu wengine wanafurahi.

Naibu Spika Dkt. Tulia Akson amesema atatoa mwongozo baada ya kufuatilia jambo hilo.

Suruali ni vazi la wanaume na sio wanawake, wanawake wanalazimisha tu kuvaa suruali, kutokana na maumbile yao ndio maana wanatakiwa wavae sketi au magauni na wanaume wavae suruali au kaptula na sio siketi,ingawa wale Waskotishi na Wazulu wanavaa sketi sio kwa wakati wote,mwananmke akivaa suruali anapata shida sana anapopata call of nature. Pamoja na hayo lakini kwa mbali naliona hili swala linaingia kwenye mtizamo wa kidini, na tusipoangalia haya mambo ya dini kuingia bungeni yatatupeleka kusiko. Nimekuwa nikiwaona wabunge wanawake wengi wakivaa suruali kama aliyovaa aliyetolewa bungeni na hawajawahi kutolewa, kwa staha hili jambo lilitakiwa lifanywe kimya kimya, naunga hoja mkono kuwa huyo dada mbunge kadhalilishwa ingekuwa amevaa jeans hapo tungeelewa lakini kwa ile suruali hata mbano hatujauona au wanataka hawa wabunge vijana wavae suruali kama za Angel Merkel wa Ujerumani?
 
Sakata la kutolewa nje kwa mbunge wa Momba, Condester Sichwale (CCM) kuhusu mavazi, limeibuka tena leo jioni katika kikao cha Bunge baada ya wabunge wanawake kutaka aombwe radhi na aliyetoa hoja.

Hata hivyo mbunge Hussein Amar amesema hawezi kuomba radhi kwa sababu alichosema alikuwa sahihi kwakuwa mavazi aliyovaa mbunge mwenzake hayakuwa na staha ndiyo maana Spika wa Bunge Job Ndugai aliridhia hoja aliyoitoa yeye (Amar).

Katika kikao cha leo jioni wabunge Jacqueline Ngonyani na Stella Manyanya waliomba mwongozo wa Spika kwa madai mbunge aliyetolewa nje alionewa.

Mapema leo Sichwale alitolewa nje kwa amri ya Spika baada ya Amar kuomba mwongozo kwa kutumia kanuni 170 kuhusu mavazi ya staha.

Ngonyani amesema kilichotokea ni kwamba mbunge huyo alionewa kwani alikuwa na vazi la staha ambalo halikuwa na shida lakini akasema huenda Spika hakuona.

"Mimi ni mjumbe wa Baraza Kuu la wanawake wa CCM, ninapoona kuna uonevu lazima niseme na hili sikiungi mkono huyu mwanamke mwenzetu ameonewa,"amesema Ngonyani.

Mbunge huyo amesisitiza kuwa uonevu wa namna hiyo haupaswi kuvumiliwa kwakuwa umemdhalilisha mbunge huyo na wapiga kura wake jimboni.

Kwa upande wake Manyanya amesema tangu asubuhi alikuwa anafuatilia kwenye mitandao na amebaini kuwa Sichwale hakuwa na vazi baya.

Hata hivyo Manyanya amesema haiwezekani wabunge vijana wavae mavazi kama wanayovaa wabunge wanawake watu wazima.

Amesema katika siku za karibuni limeibuka suala la kutoa lugha za kuwadhalilisha wabunge wanawake ndani ya ukumbi ambako wakati mwingine hutamkwa kiungo cha mwanamke halafu wengine wanafurahi.

Naibu Spika Dkt. Tulia Akson amesema atatoa mwongozo baada ya kufuatilia jambo hilo.

Hakukuwa na shida na vazi la mbunge huyo...

Ni wazi kuna shida nyingine tu binafsi za baadhi ya wabunge wa kiume na baadhi ya wanawake na Spika pasipo kujiuliza mara mbili anakubali kuingia ktk mkenge huo...

Kuna wanawake wengine wana maumbo maalumu. Hata wavaeje tu, maumbo utayaona kwa uwazi sana na kama wewe ni mwanaume usiyeweza kudhibiti hisia zako za kingono, utamtamani tu mwanamke huyo huku ukijua huwezi kumpata...

Nadhani huyu mbunge wa kiislamu alitaka huyu mwanamke akavae ushungi au baibui - lile vazi maalumu la wanawake wa kiislamu
IMG-20210601-WA0006.jpg

Hao hapo wote ni wabunge na walikuwa ndani ya bunge Jana tarehe 1/6/202. Kulia ni Catherine Maggie na wa kushoto kwako kwenye picha ni Condester Schwale...

Sichwale aliyolewa nje lakini Catherine Magige alibaki ndani ya bunge akiendelea na shughuli kama kawaida kwamba, yeye yuko vizuri...

Mimi nasema, hili sakata halihusiani na mavazi. Kuna kitu nyuma ya pazia na bahati mbaya ni kuwa uongozi wa bunge unakubali kuyumbishwa na personal interests za baadhi ya wabunge kudhalilisha baadhi ya wabunge wanawake...
 
Yule mzee ni msikiti, hivyo alitaka huyo dada avae hijabu ndio aridhike. Ila bunge futuhi nalo lina vituko vyake acha tu.

Hawa wenzetu (baadhi) ni wa ajabu sana. Wanadhani ili Mungu muumba wa vyote amkubali mwanadamu kuwa mtakatifu na Mtoto wake, basi anaangalia mavazi...

Mungu hutazama ndani ya moyo/nafsi ya mtu kama ni msafi na mkamilifu au la...

Jamaa anatamani wanawake wote wavae baibui au ushungi na kanzu ndefu hadi kwenye vidole vya miguu. Hakuna kitu kama hicho...!!

Mavazi, kwa maana mtu avae nini na kivipi inabaki siku zote ni utashi wa mtu binafsi ili mradi ni yanafunika yale maungo nyeti ya mwili wa mtu huyo vyema...

Hakuna shida kwenye vazi la yule dada. Shida iko kwenye fikra za baadhi ya wanaume ambao wanaweza kuwatamani kingono hadi mama au dada zao kwa sababu tu eti hawajafunika vichwa na nywele zao kichwani...!!

Lol, hili ni balaa kubwa kabisa...
 
Mtu mweusi mavazi yake ya asili hayakuwahi kumsitiri mwili mzima, hizi nguo sijui suti ni utamaduni wa kigeni. Sasa utaona huyo mama kavaa nguo iliyositiri sehemu kubwa ya mwili wake kinyume na zilivokuwa tamaduni za mwafrika, tuache kushobokea sana vitu ambavyo hatukuviasisi......hao wazee waseme tu uzalendo unawashinda wanapoona pisi kali zimetupia mavazi ya kisasa, wamefungwa na wakati.....
 
Back
Top Bottom