Wabunge wataka Condester Sichwale aliyetolewa nje kisa mavazi aombwe radhi

Wabunge wataka Condester Sichwale aliyetolewa nje kisa mavazi aombwe radhi

Huyu mbunge wangu naona sasa kazi imemshinda, watu wake wa jimbo tuna changamoto nyingi mfano maji vijiji vingi havina maji mradi wa maji kutoka ziwa victoria pale nyamtukuza haujakamilia sasa kageukia kuangalia akinadada wamevaa nini bungeni badala ya kusimamia hoja za msingi juu ya wananchi wake
Huyo ni mzee wa chabo!
 
wabunge wote wapuuzi tu wanashindwa kujadili vitu vya msingi kwa Taifa lakini wanabaki kijadili upumbavu tu wa mtu mmoja

Sent from my Infinix X682B using JamiiForums mobile app
 
Sisi tulishauri wabunge washonewe uniform kama student wavae sare Ili kuepusha haya awakusikia
Kama wabunge wa chama cha EFF cha Julius Malema wa SA wana uniforms zao, "overall" na kofia.
 
Kwa hiyo kila apatapo nafasi ya kuongea AONGELEE MRADI WENU WA MAJI hata kama hoja mezani ni MADINI ama WIZARA YA MICHEZO ?!!!
Mi sijamaanisha aongelee maji tu ila kikubwa hata kama ni wizara tofauti na wiazara ya maji achangie mjadala achane na mambo hayo ya mavazi tofauti na hapo atayapata majibu kwa wananchi 2025.
 
Mi sijamaanisha aongelee maji tu ila kikubwa hata kama ni wizara tofauti na wiazara ya maji achangie mjadala achane na mambo hayo ya mavazi tofauti na hapo atayapata majibu kwa wananchi 2025.
Miaka 5 ni mingi Kwani toka aingie amekuwa akiongelea hayo Mambo ya "mavazi"?!!!

Mkuu mmoja wa wapiga kura ni wewe haya msubiri ukamhukumu 2025 kwa hilo kosa la kuongelea mavazi 🤣🤣
👍
 
Ndugai ndiyo anatakiwa amuombe msamaha huyo Dada.
1622640809912.png
 
Wakuu wanaJF, mimi nadhani yule Mbunge aliyeomba mwongozo angetumia busara na hekima za kiutu uzima kwa kumueleza Spika juu ya jambo lile baada ya kikao cha bunge. Hivyo Spika angelitatua bila aibu hii ambayo tayari imo ndani ya HANSARD.
 
Kwani spika alimtoa nje kwa utashi wake au kwa mujibu wa kanuni za bunge.....?? Na hata aliyeomba muongozo aliomba kwa mujibu wa kanuni za bunge.....
Alimtoa kwa kanuni za bunge
Lakini ukiangalia syo yeye pekee
Mule aliyevaa vile

Ova
 
Watangazaze mgomo wakulala nae kimapenzi pale akiwahitaji kingono ,very easy
 
Kwa nini mbunge huyo atake huyo dada tu ndio avae vazi la Kiislam ?!!!

Na kwanini iwe jana tu ikiwa siku zote huwa anamuona ?!!

Ama siku nyinginezo huyo mh.Condester huwa anavaa hilo vazi la Kiislam alitakalo mbunge wa Nyang'wahale kiasi kwamba huridhika nafsi yake ?!!!

Je alipoomba mwongozo wa kikanuni na ikiwa SPIKA hajaukubali ,mbunge Condester angetolewa nje?!!

Je mbunge Condester ametolewa nje na mbunge wa Nyang'wahale ama na KITI cha mh.Spika?!!!
Asante sana..

Mimi nimetoa maoni yangu tu kwa namna nionavyo...

Narudia kusema tena, hayo ni maoni yangu. Naweza kuwa sahihi au wrong...

Nawe unaweza kusema kwa namna uonavyo/unavyoliona jambo...
 
Kwa mtazamo wangu nimeona pana aidha:-
1. Ushabiki wa vilabu vya Simba na Yanga. Kumbuka Spika ni kama si mwanachama basi ni shabiki kindakindaki wa klabu ya Simba.
2. Mfumo dume. Hapa na maana mtoa hoja kwa sababu zake tu ni mwanaume na Spika ni mwanaume nae hakumwangusha, angelikuwa Spika ni jinsia ya kike angejiridhisha kwanza kabla ya kutoa maamuzi.
Inawezekana...

Lakini all in all, binafsi sioni tatizo la mavazi aliyovaa mama huyo...
 
Back
Top Bottom