Leo hii inapita kabisa muda katika bunge letu tukufu linajadili kama gongo kuhalalishwa ni sahihi au la. Mwisho wa siku kila mtu anavuta mshiko wake anaelekea nyumbani. Haya hebu tuangalie mambo ya maana yanayowalenga wananchi ambayo yalihitaji muda pale bungeni......
1. Hivi jamani last time nilipocheki nyumbani, umeme ulikuwa bado ni agenda ya nani amfunge paka kengele, watu wanaogopana kuelezana ukweli kuhusu mambo muhimu ya maendeleo ya nchi yetu.
2. Usafiri ndo kizungumkuti kabisa, hata barabara za hiyo tunayoisema miji mikubwa bado ni kichekesho. Sijataja huko kunakoliletea Taifa hili maendeleo, 'vijijini'. Ukisikia Kilo moja ya mahindi inavyopata shida kupatikana utaona huruma. Kwanza mkulima hana pembejeo, akijikamua kupata angalau zinahosika, kasheshe kuisafirisha, kuileta kwa walaji, akijikamua kuileta analanguliwa bei na wajanja wa mjini.
3.Kazi hazipatikani, kama huna mjomba, shangazi, mtoto wa baba mdogo au jamaa basi wewe kibarua ni kupiga malapa na kuchapisha CV nyingi tu.
4.Ubadhirifu wa mali za umma ndo imekuwa fasheni, kama hujatafuna mali ya umma wewe si mwanasiasa mahiri, basi almuradi ni udhia tu.
Anyway nisiendeleze lawama zaidi ila leo kuhalalisha Gongo ndo muhimu....haya tena yangu macho tu...