Kwenye gongo kuna Ethanol ambayo ndo Ulabu wenyewe na kuna Methanol ambayo ni sumu japo ina test na kunukia kama ulabu.
http://en.wikipedia.org/wiki/Methanol
Ili kuhalalisha Gongo ni lazima kufanya Fractional Distillation ili kuiondoa methanol na kuiacha ethanol.
Kitu kikubwa cha kuongezea kwenye mtambo wa gongo asilia ili kufanya Fractional Distillation ni Thermometer tu.
Mafisadi wanajiuliza Gongo likitolewa sumu huko mitaani na kuuzwa kila kona nani atakunywa Konyagi?
Methanol itumike kama Biofuel na Ethanol itumike kama ulabu.
Kangara inabakiza Step 1 au 2 kuwa Bia, vilevile Gongo ambayo inajulikana kama Machozi ya simba, supu ya mawe, chang'aa, moonshine au pombe ya moshi nayo inabakiza step moja tu ili iingie kwenye kundi la Vodka Konyagi na Martin.
Waganda tayari wanabadiri gongo kuwa pombe isiyokuwa na madhara.
Uharamu wa Gongo ni kile kiwango cha Methanol kilichomo na si vinginevyo. Kama kuna sababu nyingine ni za kisiasa.