Wabunge watatu wa ajali ya Dodoma wahamishiwa MOI

Wabunge watatu wa ajali ya Dodoma wahamishiwa MOI

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Wakuu!

Ile ajali ya wabunge ukitazama kama ilikuwa ndogo lakini baadhi ya wabunge hali zao bado ni mbaya hadi wamehamishiwa MOI au tuseme maombi ya baadhi a wabongo?
=====================

Wabunge watatu majeruhi wa ajali ya basi la Kampuni ya Shabiby waliokuwa wamelazwa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, wamehamishiwa katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili-MOI kwa matibabu zaidi.

Desemba 6 mwaka huu, wabunge 16, maofisa wawili wa Bunge na dereva wa basi hilo walijeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Mbande, wilayani Kongwa baada ya basi walilokuwa wakisafiria kwenda kwenye michezo ya Afrika Mashariki, Mombasa nchini Kenya, kugongana na lori lililokuwa likitoa Morogoro kuelekea Dodoma.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumanne, Desemba 10, 2024 Meneja Mawasiliano MOI, Patrick Mvungi amesema wamepokea wabunge watatu kwa ajili ya matibabu zaidi.

Pia, Soma: Dodoma: Basi lililobeba Wabunge wa Tanzania lagonga Lori na kuwajeruhi Wabunge 23

Mvungi amewataja wabunge hao kuwa ni Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Zanzibar, Mwanakhamis Kassim Said, Mwakilishi wa Jimbo la Amani Zanzibar, Abdul Yusufu Maalim pamoja na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mwanza, Furaha Matondo.

Vilevile wabunge wengine 13 waliokuwa wamelazwa katika Hospitali ya Kanda ya Benjamini Mkapa baada ya kupata ajali hiyo wameruhusiwa baada ya kupata matibabu.

Snapinsta.app_469714781_583513877697704_3564896812538900698_n_1080.jpg
Snapinsta.app_469712862_1297710477911216_6311570611466416245_n_1080.jpg
 
Kwa kawaida ikitokea ajali, Jeshi la Polisi huwataja kwa majina, Umri, kabila pamoja na Makazi wahanga wote wa ajali.

Kwa wabunge wetu naona ni tofauti. Wahanga hawatajwi, na hata chanzo cha ajali sijasikia kikitajwa na Polisi wetu..
 
Desemba 6 mwaka huu, wabunge 16, maofisa wawili wa Bunge na dereva wa basi hilo walijeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Mbande, wilayani Kongwa baada ya basi walilokuwa wakisafiria kwenda kwenye michezo ya Afrika Mashariki, Mombasa nchini Kenya, kugongana na lori lililokuwa likitoa Morogoro kuelekea Dodoma.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumanne, Desemba 10, 2024 Meneja Mawasiliano MOI, Patrick Mvungi amesema wamepokea wabunge watatu kwa ajili ya matibabu zaidi.
Yote aachiwe Mungu
 
Back
Top Bottom