Tetesi: Wabunge wawili, watahama upinzani punde

Tetesi: Wabunge wawili, watahama upinzani punde

Tatizo la baadhi ya wabunge ni kuwa na mipango ya baadae katika maeneo yao ila si mipango ya kuwaletea maendeleo wananchi. Wabunge wanakuwa wafanyabiashara na dili mbalimbali ndio maana mambo yanasimama.
 
Halijafungwa na liko wazi sana ila hawataruhusiwa kugombea kwa tiketi ya CCM.
Usajili wenu mnafanyia wapi sasahivi maana ni kweli mlifunga usajili. Tumtafute Msemaji wa CCM atudokeze utaratibu unakuwaje endapo kweli hili litajitokeza
 
JUZI MMETULETEA HABARI KUWA MMEMKATAA MBUNGE MACHACHARI WA CHADEMA ALIYETAKA KUHAMIA KWENU, LEO TENA MNATULETEA HABARI WABUNGE MACHACHARI WANATAKA KUHAMIA KWENU. HIVI MNAFIKIRI SISI HATUNA KUMBUKUMBU
 
Hakuna kitu kama hicho hadi dirisha kubwa la usajili
Wanabodi,

Kama ilivyo ada, ninawaletea habari mpya, ambayo ina msisimko kwa siasa za nchi kwa sasa. Jana majira ya saa 7 mchana niliipata ila imethibitishwa leo asubuhi. Wabunge wengine 2(wenye majina makubwa) wataondoka Upinzani na kujiunga na CCM ama kuacha siasa. Malengo yao ni kujipanga kwa ajili ya 2020.

Swali langu, hamahama itakwisha lini tujenge nchi?

Nelson,
Mwanza
 
Imekua kama mchezo vile hawaoni taifa linavopoteza fedha kufanyia uchaguzi kila kukicha
 
Kwa hiyo watakubali 2019 yote ipite kavu kavu, au kutakuwa na namna?

Naomba kama una jibu jibu kama huna kaa kimya, sio uje uniambie nikamuulize Mr Slow slow.
Kama alivuofanya nyalandu kukubali 2018,2019 kupita kavukavu
 
Back
Top Bottom