Wachache wanaojitoa kuelezea mapungufu ya Magufuli, wana msaada mkubwa kwa Taifa kuliko mamia au maelfu walio huru kueleza mazuri yake

Wachache wanaojitoa kuelezea mapungufu ya Magufuli, wana msaada mkubwa kwa Taifa kuliko mamia au maelfu walio huru kueleza mazuri yake

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,828
Reaction score
165,667
Habari wakuu,

Ni hivi: Ingekuwa ni jambo la hatari sana kama kila mtu angejitoa akili (angejisahaulisha) kuhusu mapungufu ya Marehemu Magufuli na utawala wake na kisha wote tungeungana katika kusifu pamoja na kuendesha hizi propaganda zinazoendelea kwa kutumia vyombo vya habari.

Ukweli ni kwamba, Magufuli kama binadamu wengine, alikuwa na mapungufu yake ambayo leo hii kuyatamka au kuyaongea hadharani kunahitaji kujitoa.

Hatari iliyopo ni kuwa, kama wote tungeamua kujitia upofu na tukaongelea mazuri tu ya Magufuli, kuna uwezekano mkubwa viongozi wengine wakaiga kufanya mabaya wakiamini jamii huyapuuza na kuangalia mazuri tu.

Binafsi nina hakika wale wanaotumia mitandao kueleza maovu ya watawala hata baada ya wao kufariki, wanawafanya watawala wanaobaki au kurithi madaraka kuwa na woga wa kuja kusemwa vibaya pindi watapofariki iwapo watatendea watu uovu au kutumia madaraka yao vibaya.

Na hapa naomba niseme wazi kuwa yule Bwana kule twitter anaeonekana mkorofi, hana utu, si mzalendo, n.k, Bwana huyu ana msaada mkubwa sana leo hii kuliko wale waliojikita katika kusifu na kupongeza tu.Anachofanya huyu Bwana ni kuwapa somo na pia woga viongozi wengine kufanya mambo mabaya kwa hofu ya kuja kusemwa au kuandikwa vibaya pale watapoitwa mbele za haki, na mwisho wa siku anaefaidika ni mwananchi wa kawaida anaetambulika kama mnyonge.

Hivyo,wale wanaosema yale ambayo baadhi ya watu leo hii hawataki kusyasikia, watu hawa wanasaidia sana ku-shape viongozi wanaobaki kwa faida ya Taifa zima na watu wake, na wana msaada mkubwa sana kwa nchi na watu wake kuliko wale waliochagua kusifu na kupongeza tu huku wakijisahaulisha kabisa mapungufu ya wale viongozi walioitwa mbele za haki na hata wale walio hai.

Kumbukeni kila jambo huwa na sababu, hivyo mtafakari kwani hili limetokea na zaidi kwanini tumekuwa na mtu kama yule kule twitter katika utawala huu au katika kipindi hiki.

Kwa kifupi, jiulize kama ni coincidence tu au ni mipango ya Mungu?

Mwisho, mnaomsifu marehemu mmengekuwa wa maana zaidi na wenye msaada kwa marehemu kama mngekiri alikuwa na mapungufu na mkatumia muda wenu kumuomba kwa Mungu amsamehe kwa yale aliyokosea.
 
Tukidanganya kwamba alisaidia wanyonge kwa hali kama hii ni kuficha mambo bila sababu ya msingi

Picha: Huyu ni muuza madafu akiwa chini ya ulinzi wa Mgambo baada ya kukamatwa kwa tuhuma za kufanya biashara bila kitambulisho cha mmachinga ambacho gharama yake ni tsh elfu 20

2082683_FB_IMG_1559946076802.jpg
 
Tatizo tunatishana Sana , mambo mengine tumwachie Mungu Tu sasa aongoze yeye
 
Endeleeni tu "kukazana" na yule jamaa kule "twita". Watanzania tunampumzisha shujaa wetu leo.
 
Tukidanganya kwamba alisaidia wanyonge kwa hali kama hii ni kuficha mambo bila sababu ya msingi

Picha : Huyu ni muuza madafu akiwa chini ya ulinzi wa Mgambo baada ya kukamatwa kwa tuhuma za kufanya biashara bila kitambulisho cha mmachinga ambacho gharama yake ni tsh elfu 20

View attachment 1734731
Mambo kama haya wao hawatki kuyasikia wala kuyaona ingawa yalitendeka.
 
Hizi kejeli zote zina mwisho, tutamzika shujaa wetu then tutahakikisha kila mtu anapata stahili yake iliyo halali, Lissu anarudi lini Tanzania na yeye apate stahili yake?
 
Hamna aliyewakataza, fungukeni na toeni ya moyoni mwenu, tunachojua watanzania wengi yapata asilimia 85 walimuunga mkono na kukubaliana na njia zake za kutetea maslahi ya taifa.

Hata yeye alishasemaga hajaja kuuza sura, anajua anapendwa mke wake na watanzania wengi hivyo wale wachache pia ni haki yao kumchukia.
 
Halafu niulize hivi unyonge na IQ hafifu zinaendana?

Kuwa maana kunamambo ya kushangaza yanaendelea

Kuna mnyonge kaja kwangu huku akisifusifu juhudi za Madaraja atanikuta napiga Konyagi zangu

Akaniambia anywe kidogo kwa ajili ya msiba wa kupoteza Chuma (yaani Magu) chake

Chaajabu baada ya kugida glasi nzima ya Gin anamgeukia Marehemu (Magu)na kumshutumu kwa umasikini wake kitu ambacho kimempelekea kuenga mabanda ya Kuku wakati angelikuwa na kazi maalumu 😁
 
Hamna aliyewakataza, fungukeni na toeni ya moyoni mwenu, tunachojua watanzania wengi yapata asilimia 85 walimuunga mkono na kukubaliana na njia zake za kutetea maslahi ya taifa...
Hata yeye alishasemaga hajaja kuuza sura, anajua anapendwa mke wake na watanzania wengi hivyo wale wachache pia ni haki yao kumchukia.
Kumbuka tu watu waliopotezwa na watu wasiojilikana, hawakupata hata nafasi ya kuombewa na kuagwa na ndugu na jamaa zao, bali walitupwa baharini wakaliwe na samaki.
 
Usitake kutufanya kwamba watanzania hatuna akili ya kuchambua mbichi na mbivu, kuzuri na kibaya au pa kusifu na pa kukosoa.

Magufuli anasifiwa, au sifa kubwa ya Magufuli iliyofanya apate umaarufu huu alionao hata baada ya kutangulia mbele za haki ni kwamba alionyesha moyo fulani hivi, na akatenda mambo fulani hivi, yaliyogusa maelfu kwa maelfu ya watanzania.

Watanzania hatunaga hiyana, hasa akiwa kiongozi -- yeyote atakeyafanya vizuri atakaa mioyoni mwetu, na yeyote atakayefanya vibaya atapuuzwa tu.

Pia tofautisha kukosoa (constructive criticism), na kufanya fujo (detractors). Yule mkosoaji mkubwa wa Magufuli kuna wakati tu alionekana /anaonekana wa hulka ya kufanya fujo tu, hajui wakati gani pa kukaa kimya achunguze kinachoendelea, au wakati gani atoe hizo criticism zake.
 
Tukidanganya kwamba alisaidia wanyonge kwa hali kama hii ni kuficha mambo bila sababu ya msingi

Picha : Huyu ni muuza madafu akiwa chini ya ulinzi wa Mgambo baada ya kukamatwa kwa tuhuma za kufanya biashara bila kitambulisho cha mmachinga ambacho gharama yake ni tsh elfu 20

View attachment 1734731
Mataga watakwambia muuza madafu alikuwa anaselfika na mambo
 
Hizi kejeli zote zina mwisho, tutamzika shujaa wetu , then tutahakikisha kila mtu anapata stahili yake iliyo halali, Lissu anarudi lini Tz na yeye apate stahili yake?
Mshakatwa mikono nyinyi! Aliyewapa jeuri, ndiyo huyu tunaye mpumzisha jioni ya leo. Nyinyi uvccm wenyewe wa kipindi hiki ni mlenda mlenda tu! Mtamfanya nini huyo Lissu siku ya kurudi?

Mtaweza kweli kupambana na wale walinzi wake? 💪
 
Kumbuka tu watu waliopotezwa na watu wasiojilikana hawakupata hata nafasi ya kuombewa na kuagwa na ndugu na jamaa zao bali walitupwa baharini wakaliwe na samaki.
Haya maneno hayana ushahidi wowote. Na kama yametokea haya matukio ni ya kusikitisha ila sio ya ajabu, hata nchi zingine yanatokea. Mfano wewe kama una mtu unadhani ni mbaya wako na likakutokea jambo baya ni rahisi kumnyooshea kidole mbaya wako hata kama sio yeye...
 
Back
Top Bottom