TODAYS
JF-Expert Member
- Apr 30, 2014
- 14,747
- 24,250
Nimeshtushwa kidogo kutoka kwa huyu ndugu Kimaro.
Mkoa wa Kilimanjaro, katika kijiji cha Mbosho, wilayani Machame, kutana na Patrick Kimaro, mwenye umri wa miaka 59, ambaye amejingea kaburi lake.
Kimaro amesema ni sehemu tu ya kujiandaa na maisha ya baadae na kuongeza kusema amefanya hivyo akiwa na akili timamu bila kushinikizwa, lakini bado, kwa baadhi jambo hilo kwao linatia ukakasi.
Anasema, 'nilionja machungu baada ya kuandaa mazishi ya wazazi wangu'
Baadhi wanalichukulia kama uchuro kwa misingi kwamba linaweza kuleta kisirani katika familia.
Hatua hii ya Bwana Kimaro imewashangaza wengi, ndani ya kijiji chake na nje ya mipaka ya kijiji hicho. Kwa sababu sio jambo lililozoeleka katika jamii ya kiafrika hasa jamii ya kichagga anayotoka Kimaro.
Source: BBC