Wachaga na Wahaya ni kweli hawajui matumizi ya simu????

bornagain

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2012
Posts
3,383
Reaction score
1,360
Hivi hawa watani zangu watu wa Kilimanjaro na baadhi ya watu wa Kagera hawajui matumizi ya simu, mimi siamini hata kidogo kama hawajui matumizi ya simu kwa sababu ni watu wanaojua maendeleo na wengi wao wameelimika sana kuliko sisi wa pande za kati.

Kitu kinachonitatiza kwa hawa jamaa ni kimoja hivi kwa nini wakifiwa wasijulishane misiba kwa technologia ya simu na sio kwa kupitia radio. Utasikia mzee Masawe wa Rombo mkuu ama Rweikiza wa Kanyigo anasikitika kutangaza kifo cha mjuu wake kilichotokea hospitali ya Aga Khan habari ziwafikie sijui nani mpaka waliopo Marekani na Uingereza, sasa mimi nabaki nacheka tu ina maana huko Marekani na Uingereza nako radio zinashika kweli tena hizi radio zetu za masafa ya FM.

Tafadhari mwenye uelewa kwa nini hawa jamaa hawatumii simu kutangaza misiba anijulishe ili nisirudia tena kuuliza hili swali
 
acha hzo ndugu! Kwani ww inakukera nn hiyo tabia..!wivu huo
 
Jokes/utani+gossip/umbeya ndio mahala sahihi pa kuweka huu utumbo
 
Siku hzi Msiba ni sherehe na sherehe zina mbwembwe zake:

Chakula kutoka the best caterer, Sare za wafiwa, Muziki na Mc wa viwango, Jeneza high quality, kaburi la marumaru, official arrangement ya waombolezaji (soma - wageni waalikwa) n.k n.k.

Na tambua kama kuna Wageni wanatoka US ama Europe kunakuwa na watu maalum wa kuwapokea.

Kumbuka: Hupaswi kulia bila mpango, lia kulingana na viwango vya msiba, ukipayuka utanyamazishwa. Lia kisasa zaidi
ukiwa unatoa sauti ya chini na kama machozi yanatoka hakikisha una leso ya maana. Usisahau suti yako nyeusi pliz.
 
da noma sana aisee
 
Hahahahaah! Hii misiba ya siku hizi full balaa na kadi za michango juu.
 
binafsi nafikiri ni mazoea tu na kama radio one inasikika sana uchagani so utangazaji utawafanya wengi wapate habari, i.e bwana arkard kimario wa useri rombo anackitika kutangaza kifo cha mwanae gaspa kimario kilichotokea Mutukula kagera kikao cha maziko kitafanyikia pale Bamboo inn kuanzia sa11 jion habari ziwafikie faustine ngaleya shayo akiwa Tarakea Rombo n Expery Tarimo wa Kikombaa Nairobi.. mwili wa marehemu utapelekwa usseri kwalakamu j4
 
Back
Top Bottom