Wachagga walitaka kuunda nchi yao (Chagga State), Mwl. Nyerere akaomba wasifanye hivyo

Wachagga walitaka kuunda nchi yao (Chagga State), Mwl. Nyerere akaomba wasifanye hivyo

kama hiyo state ya wachagga ingekuwa hai mpaka leo basi watanganyika tungekuwa na mapambano ya kuvunja muungano sehemu mbili, zanzibar na chagga state.

nyerere alikuwa sahihi kuwasambaratisha hao wachagga sijui alibugi wapi kwa wazenji.

ukabila.
 
Nyerere aliwaharibia sana, imejini unaunganishwa na wauza nchi na majitu ya msoga ni laana tupu.

Wachaga wako siriazi na maisha sna sana tu.

Hawauzi hata hatua moja ya kipande cha ardhi, nafikiri Kilimanjaro ingeshindana na Dubai
Hata Wazanzibar walijichomeka sana kuungana na watu wa nchi hii. Zanzibar ingejitegemea ingekuwa mbali sana kiuchumi hata zaidi ya Kenya. Nchi hii kila alieko kwenye hafikirii chochote zaidi ya tumbo lake na ndugu zake. Mtu anaingia ofisini kichwani anafikiria namna ya kuiba tu.
Wachaga nimefanya nao biashara ni watu smart sana. Wangekuwa mbali sanaaa na nchi yao
 
kama hiyo state ya wachagga ingekuwa hai mpaka leo basi watanganyika tungekuwa na mapambano ya kuvunja muungano sehemu mbili, zanzibar na chagga state.

nyerere alikuwa sahihi kuwasambaratisha hao wachagga sijui alibugi wapi kwa wazenji.

ukabila.

..taarifa kwamba Wachaga walitaka kuunda nchi yao sio ya kweli.

..kuna taarifa rasmi za nyaraka za UN zinaonyesha Mangi Marealle na Mwalimu Nyerere wakiunga mkono Uhuru wa Tanganyika walipoitwa kwa mahojiano ktk vikao vya UN.

..Mangi Marealle aliulizwa kuhusu hadhi na nafasi ya Machifu baada ya Uhuru wa Tanganyika na alijibu anatarajia tutafuata mfano Machifu wa Ghana.
 
Mwandishi amekusudia kupotosha ukweli. Mbona hajaeleza uhasama Kati ya Wakibosho na Wamachame.
 
Hata Wazanzibar walijichomeka sana kuungana na watu wa nchi hii. Zanzibar ingejitegemea ingekuwa mbali sana kiuchumi hata zaidi ya Kenya. Nchi hii kila alieko kwenye hafikirii chochote zaidi ya tumbo lake na ndugu zake. Mtu anaingia ofisini kichwani anafikiria namna ya kuiba tu.
Wachaga nimefanya nao biashara ni watu smart sana. Wangekuwa mbali sanaaa na nchi yao
Wachaga nimefanya nao biashara ni watu smart sana. Wangekuwa mbali sanaaa na nchi yao[emoji419][emoji375]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
By then (moshi) kilimanjaro ilikuwa mbali sana kimaendeleo kuzidi mikoa kingine ya the then Tanganyika mwalimu alikosea sana kuwaita hawa jamaa wabinafsi kwa sababu kwanza sidhani kama kungekuwa na shida yoyote ya kilimanjaro kujitegemea ni falsafa za kijinga za kijamaa walizokuwa nazo waasisi wa taifa ili la kujifanya eti tupate uhuru kama nchi mbona kuna vi nchi vidogo hata kuliko mkoa wa kilimanjaro na vilipata uhuru vyenyewe ??
 
Wakati wazungu wanagawana bara la Afrika, walipokuja walikuta baadhi ya maeneo kuna tawala zenye nguvu, zilizokua na mfumo rasmi wa uongozi.

Mojawapo ya tawala ilikuwa ni dola ya wachagga (Chagga state). Dola hiii ilikuwa na Kiongozi Mmoja aliyeitwa Mangi Mkuu

Mangi mkuu aliteua Mamangi wadogo wadogo (RC, DC) mfano Mangi Meli wa Old Moshi, Mangi Sina wa Kibosho, Mangi Salakana wa Useri etc.

January 1952 kulifanyika uchaguzi wa kumchagua Mangi Mkuu wa Wachagga. Wagombea walikua watano. Abdieli Shangali wa Machame, Jackson Kitali wa Mbokomu, Petro Marealle, John Maruma na Thomas Marealle. Thomas Marealle aliibuka Mshindi katika Uchaguzi huo

Turudi nyuma Kidogo, mwaka 1920 dola ya wachagga ilikua ya kwanza Afrika Mashariki kuanzisha na kumiliki gazeti lake (Komkya).

Huduma za maji, umeme, miundombinu ya barabara, hospitali na shule vilifika mapema kulinganisha na maeneo mengine ya nchi. Ikulu ya kisasa ya Mangi Mkuu wa wachagga, iliyojengwa miaka hiyo hadi sasa ndio Ikulu ndogo ya Rais kwa mkoa wa Kilimanjaro.

Maendeleo haya na mengine mengi, wachagga waliamini yalitokana na elimu. Kwahiyo mwamko wa elimu ulikua mkubwa hasa baada ya wamisionari kujenga shule na huduma za afya kila walipojenga kanisa. Vitu hivi vitatu viliambatana. Kanisa, Shule, na Kituo cha afya.

Kwahiyo hata kwenye kuchagua viongozi, yule aliyekuwa na elimu nzuri ndiye aliyepewa nafasi kubwa ya kushinda ikiaminika kwamba elimu yake itachochea kasiYa maendeleo..Na hii ni moja ya sababu iliyomfanya Thomas Marealle kushinda kiti cha umangi mkuu mwaka 1952, kwani kati ya wagombea wote yeye ndiye aliyekua na shahada ya uzamili (masters degree) kwa wakati huo.

Kabla ya uhuru kulikua wachumi wawili tu wazawa ambao ni Thomas Marealle na Fredrick Mchauru ambaye walisoma pamoja London School of Economics, kabla ya Marealle kupata ufadhili Cambridge University.

Uingereza ilitaka dola ya wachagga ijitenge kutoka Tanganyika na itafute uhuru wake yenyewe,
Hata hivyo mpango huo ulishindikana kwa kuwa Tanganyika ilikua 'Trusteeship colony' ya Umoja wa mataifa, na Uingereza alikabidhiwa tu aisimamie hadi iweze kujitawala.

Kwahiyo hoja ya Muingereza ilitupwa kwa maelezo kwamba wakati wa kugawanya bara la Afrika pale Berlin mwaka1884/85 hakuna nchi inayoitwa 'Chagga state's iliyogawanywa. Shirika la ujasusi la Uingereza (M16) lilimpendekeza Mangi Thomas Mareale kuwa Rais wa kwanza wa Tanganyika baada ya uhuru kutokana na umahiri wake katika uongozi lakini Marealle hakuwa na ushawishi mkubwa kwa makabilaMengine nje ya wachagga. Na hii ni moja ya hofu kubwa aliyokua nayo Mwalimu Nyerere wakati wa kudai uhuru. Alipofika uchaggani alikuta dola ya wachagga ina mamlaka kamili. Ilikua na 'well defined leadership structure', bendera yake, wimbo wake, na askari wake. Nyerere alisema Ili Tanganyika iwe uhuru lazima dola ya wachagga ife kwanza, kwa sababu hatuwezi kuwa na taifa moja ndani ya taifa jingine.

Mwaka 1961 Nyerere aliagiza bendera ya Tanganyika isipandishwe kabla bendera ya wachagga haijashushwa kwanza.

Hata hivyo hofu ya Nyerere haikua na mashiko kwa sababu Mareale alimpa ushirikiano mkubwa wakati wa kudai Uhuru. Na ili kuonesha kwamba hakuwa na mpango wowote wa kumhujumu, aliamua kujiuzulu nafasi yake ya umangi mkuu mwaka 1960, na kuruhusu askari wake kujiunga na jeshi la Tanganyika.

View attachment 2668575View attachment 2668576View attachment 2668577

Sent using Jamii Forums mobile app
Sio kitu cha ajabu watu kujitenga,
India,Pakistan,Bangladesh ilikuwa nchi moja,zikajitenga,waislam upande mmoja,wahindu mmoja,
Tribal wars,ni kawaida tu,kuna kabila la wakurd,wapo Iraq,wapo Turkey,na wanataka kujitenga wawe nchi kamili.
 
By then (moshi) kilimanjaro ilikuwa mbali sana kimaendeleo kuzidi mikoa kingine ya the then Tanganyika mwalimu alikosea sana kuwaita hawa jamaa wabinafsi kwa sababu kwanza sidhani kama kungekuwa na shida yoyote ya kilimanjaro kujitegemea ni falsafa za kijinga za kijamaa walizokuwa nazo waasisi wa taifa ili la kujifanya eti tupate uhuru kama nchi mbona kuna vi nchi vidogo hata kuliko mkoa wa kilimanjaro na vilipata uhuru vyenyewe ??
What is to stop wale wanauzunguka Mlima pekee au mto fulani pekee kuunda nchi yao ? Haya ni mawazo ya mtu ambaye hajui nguvu ya umoja na mwisho wa siku anaweza kusema sababu mtaa fulani umeendelea sana basi tujitenge tuwe mkoa tuondokane na mtaa ule ambao ni masikini....

Naweza kusema mawazo kama yako ni kutokuangalia the whole equation; unaangalia pros to bila cons...
 
Eeeeeh....Vya nyumbani haviibiwi kamwe...
MAANA VINAPIGWA MORO VINAENDA MLIMANI, UNAKUMBUKA MZEE WA KIRARACHA, ANAKUKAMATA MTWARA, ANAKUAGIZA MKUTANE VUNJO, SASA VUNJO NA IKULU WAPI NA WAPI. HATARI NA NUSU
 
Baadhi ya picha zinazoonyesha tawala za dola ya wachaha enzi hizo

IMG_1115.jpg

IMG_1114.jpg

IMG_1112.jpg

IMG_1111.jpg

IMG_1113.jpg
 
Back
Top Bottom