Asante sana!
Wewe una mawazo kama yangu kila mahali. Pia nilikuwa natafuta jina la huyo Kashasha, nilisahau jina lake, nilimuona Tbc nikapiga saluti. Kwa Tz, kwangu huyu ndo namba moja. Umeongea ya Dr. Leakey, uko sawa kabisa na pia nafikiri watu wanamkubali sababu ni mmoja wa wachambuzi wa kwanza kuanza onekana ktk tv enzi za dtv na premier ligi enzi zile, ila hayupo technically au tactically kabisa. Yeye likifungwa goli atakumbushia kwa kulilinganisha na goli lililofungwa kipindi fulani. Kiufupi ni mzee wa historia ktk matukio ya soka. Edo na Leah wanajitahidi sana, bado vijana ila Dauda ni majungu na kuponda, bado sana!