Kuweka rekodi sawa: Ujeremani waliwafunga Saudi Arabia goli nane mwaka 2002 na sio 2006.dr rick 2006 alipoulizwa nan atawin world cup bila hofu akasema italy huku ikiwa ya mwisho kundini imefungwa mechi moja na kusuruu moja na mech iliyosalia dhid ya german ambayo imempiga saudia goli nane italy wakashinda game ya mwisho na mwisho wwkafika finnal hapo ndio nilipomfaham rick abdala mzee wa mikeka mfolow insta na fb muone mikeka yake coz ananipa sana hela ya kula
Asante sana!
Wewe una mawazo kama yangu kila mahali. Pia nilikuwa natafuta jina la huyo Kashasha, nilisahau jina lake, nilimuona Tbc nikapiga saluti. Kwa Tz, kwangu huyu ndo namba moja. Umeongea ya Dr. Leakey, uko sawa kabisa na pia nafikiri watu wanamkubali sababu ni mmoja wa wachambuzi wa kwanza kuanza onekana ktk tv enzi za dtv na premier ligi enzi zile, ila hayupo technically au tactically kabisa. Yeye likifungwa goli atakumbushia kwa kulilinganisha na goli lililofungwa kipindi fulani. Kiufupi ni mzee wa historia ktk matukio ya soka. Edo na Leah wanajitahidi sana, bado vijana ila Dauda ni majungu na kuponda, bado sana!
Kati ya wooote hao no1 ni dr no2 manara waliobakia wooote ni wachumia tumbo
Dr. Leaky uchabuzi wake haupo technically sana kama ulishamfuatilia vizuri. Yeye anaweza kutoa historia pia na reaction za mashabiki kwa timu fulani. Pia kinachoonekana anajua kuchambua ni kwasababu anapenda sana mpira na ni mmoja ya watanzania ambaye mara nyingi anaweza kusafiri kwenda Ulaya kuangalia gemu fulani mfano hizi za Champions League au Euro na WC. Kwahiyo uzoefu wake ndio unasabaisha hivyo.
Lakini kwenye ufundi zaidi Mwl. Kashasha ni zaidi ya wote kwa mtazamo wangu. Yule mzee nimemfuatilia sana. Akiangalia mpira dakika 15 tu anaweza kutabiri timu inafungwa kama haitabadili mfumo fulani. Aisee jaribu kumfuatilia huyu mzee huwa ananipa raha sana jinsi alivyo technically.
Eddo Kumwembe pia ni mzuri
Jeff Leya nae ni mzuri
Manara namkubali
Shafii Dauda bado sana huyu
Huyo Dr.??Ricky ni mjanja wa mjini ambae hukariri habari za soka toka mitandao mbalimbali ya michezo toka ulaya na kuja kuwakoga watu mbele ya TV ambao humuona ni mjuzi wa mambo ya soka wakati ni wa kawaida tu.
Hata Shaffi nae yupo kama
Rick(sio Leakey) japo huyu huwa anajiongeza kuipa maana ya kile anachokichambua.
Hawa ndio the best;
1.Eddo
2.Kashasha.
Kinachonifanya namba 1 nimpe Shafi Dauda yuko deep sana ao wengine naona wanapita tu juujuu
Naomba CV ya Mwl.Kashasha1. Dr Ricky
2. Edo kumwembe
3. Maestro
4. Haji manara
5. Shafii dauda
We list yako ya 5 bora ya wachambuzi wa soka nchini ni ipi?