FYATU
JF-Expert Member
- Dec 7, 2011
- 5,882
- 5,087
Kwamba ndio italeta usawa kwenye ligi,hapana nakataa. Yapo mengi tu ya kurekebisha yanayokiukwa kuleta usawa badala ya kulazimisha wenzenu wakaungua na jua eti huo ndio usawa.Huo usawa roho mbaya?.
Mmekuwa kama chongo anayetamani Mwingine naye apoteze jicho ndio aone wapo sawa.Kama kucheza mchana kunauma basi namna nzuri ya kupata usawa ni ya kuwaombea wale wanaocheza mchana watoke huko.
Na kwa hoja ya kibiashara kama inavyoelezwa,mbona ina mashiko sana tu, msichoelewa hapo ni nini?
.Kwa nini msiendeshe kampeni mechi zote za ligi zifikie kuleta mapato saw kama za Simba na Yanga?.kwamba hata huku mtaani siku wanacheza Prison na KMC basi hata vibanda umiza vifunguliwe tofauti na sasa ili kumjua Mchezaji wa Kagera sugar ni mpaka mechi yao na Simba au Yanga.
Kama Azam anatoa pesa kwa timu zote kwa nini muendeshe kampeni ya kumpunguzia mapato na si kuongeza?.Hizo timu zitakuwa tayari kupunguziwa mgao iwapo mapato ya Azam yatapungua? Kama Simba na Yanga ndio "Wanyama kazi"wa mapato ya ligi kwa sasa kwa nini tusikubali ukubwa wao huo mpaka hapo itakavyokuwa vinginevyo?.
Nitawaelewa kama mtaendesha kampeni kila mkoa uwe na Kiwanja cha kisasa timu zicheze hata usiku badala ya mchana unaoumiza,pia kuwe na Kampeni Viwanja vijae hata kama wanaxheza JKT na Kengold li Azam apate pesa ya kuwalipa timu shiriki, au wafanye mnavyotaka nyie alafu pesa achukue kwenye mapato ya ice cream?.
Kwamba mnatulinganisha na England,kweli? England kule ambako hata wakicheza SouthHsmpton na Barnley uwanja unajaa vile vile wanavyojaza Man U?Hampo serious.
Narudia tena usawa si mpaka wote mteseke mnaweza kupambana wote mneemeke.