Tuwachambue wachambuzi wetu wa soka
Nasikia wanaingia sana JF kusikilizia pale tunapo wachambua na wao
Mimi naanza na wachambuzi wa Clouds Media haswa Sports Extra
WAONGOZAJI ni
Prisca Kishamba
Alex Lwambano
Mkazuzu
WACHAMBUZI
Shafii Dauda
Edgar Kibwana
Coutinho
Yahaya Njenge
Amri Kihemba
Privaldinho
Faram Kihamwe
Issa Marda
James Turpa Turpa
RIPOTA
Mkomwa
Kwa waongozaji sina neno nao sana wanajitahidi ingawaje Prisca anaoneka mweupe kiaina na Lwambano ni mswahili sana(anafurahisha) yaani huwa anawakilisha mawazo ya wale mashabiki wa kawaida kabisa kwa jinsi anayofanyaga assumptions zake
WACHAMBUZI
Privaldinho
Itoshe tu kusema hamna kitu pale zaidi ya kuremba remba sauti na ujuaji
Haka kajamaa bora kaende tu kwenye field yake ya sheria, huku miyeyusho sana
Coutinho
Huyu anaijua vizuri sana basketball na yuko vizuri kuichambua
Ni mmoja wa wachambuzi wa ki theory zaidi kuliko FACTS, anaonekana yupo vizuri ila anakuaga bias linapokuja swala la Liverpool
Edgar Kibwana
Mzee wa what a game, what a come back, what a goal[emoji23][emoji23]
Huyu bwana kwa kutaja kiufasaha majina ya vilabu haswa vya italiano mbona utampenda
Kiujumla ni mjanja mjanja flani hivi kwenye uchambuzi na ana vitakwimu fulani hivi
Yahya Njenge, Farahn Kihamwe na Issa Maeda
Hawani ni aina ya wachambuzi wa kujenga sana theory kuliko uhalisia
Wakianza porojo za kwa nini Simba haifungi yaani atatengeneza equation, formula, ikapanda ikashuka sijui mfumo tactical effect yaani blah blah mingiiiii
Amri Kiemba
Huyu ndio mtu pekee pale clouds media anajua kuchambua mpira wa miguu kwa FACTS au Professional opinion.
Ligi ya kibongo anachambua kwa fact haswa nakitaalamu bila kuvuta maneno mengii, anakua mtamu zaidi muongozaji akiwa Lwambano halafu aanze kumchagiza kuhusu ligi za bongo na figisu zake
Shaffi Dauda
Mzee wa controversial
Ujuaji mwingii
Anaweza akatoa mtazamo wake bongo nzima ikasimama kumjadili, akina Manara wataitisha hadi na media
anajitahidi kiasi chake
James Turpa Turpa[emoji23][emoji23]
Huyu jamaa ni comedian
Kama unataka kupata habari za michezo kikomedi basi huyu jamaa atakufaa
Mkomwa
Huyu mshkaji ni ripota mzuri sana kwenye vijiwe vya maahabiki na wauza magazeti
Nini maoni yako?