Halafu sema tu mashabiki hamna kumbukumbu
Timu yenu inapopata matokeo mabovu, nyinyi ndio mnakuwa wakwanza kuwanyooshea wachezaji vidole kabla hata ya wachambuzi
Labda kama hufatiliagi interviews za mashabiki baada ya game
Huyo Lomalisa, Morrison hadi Aziz Ki wote walishawahi kusemwa kuwa hawajitumi kama ambavyo walivyokuwa wanacheza kwenye Club zao waliko tokea
Hayo maneno yalisemwa na nyinyi mashabiki
Na hii ni kawaida, ipo hata kwa Simba, kitu nachokiona hapa ni kwamba nyinyi mashabiki ni kama ndio mna uhalali wa kuisema timu yenu vile mtakavyo, ila maneno hayo yakisemwa na mchambuzi tayari inakuwa nongwa, mchambuzi fulani ana chuki
Mimi napenda kusikiliza Dunia ya michezo wapo Radio, pale kuna mchambuzi anaitwa Salumu Mnolela, yule anasema kabisa kuwa Simba mbovu na anakupa na sababu. Simba haina kikosi kipana, Quality ya mchezaji mmoja mmoja bado ni tatizo na mimi namkubalia na pia nakumkubali kama mchambuzi mzuri.
Wala sioni kama hiyo ni chuki kwasababu anachokiongea kinaonekana, so siwezi kutafuta kimechi kimoja kama kile cha Mtibwa nikashinda goli 5 afu nikakitumia hicho kuanza kumsema Salum Mnolela kuwa ni mnafki anachuki na Simba kwasababu kikosi alichosema kibovu kimeshinda bao 5.
Maoni ya wachambuzi yaheshimiwe japo hayawezi kuwa sahihi ila please tusiwajengee chuki. Tutawafanya wawe wanalazimika kuongea unafki ili tu kuturidhisha mashabiki.