Wachambuzi uchwara vipi, Lomalisa bado tumepigwa?

technically

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2016
Posts
12,706
Reaction score
52,355
Mechi ya tatu mfululizo dogo anakiwasha kisawasawa, kuanzia Tunisia, kule Mwanza na leo uwanja wa taifa. Wachambuzi wa bongo Lomalisa anawavua nguo!

Ushauri katika uchambuzi wenu lazima muwe mnaweka akiba ya maneno.
 
Ya warabu Tunisia 😀😀😀😀
Halafu sema tu mashabiki hamna kumbukumbu

Timu yenu inapopata matokeo mabovu, nyinyi ndio mnakuwa wakwanza kuwanyooshea wachezaji vidole kabla hata ya wachambuzi

Labda kama hufatiliagi interviews za mashabiki baada ya game

Huyo Lomalisa, Morrison hadi Aziz Ki wote walishawahi kusemwa kuwa hawajitumi kama ambavyo walivyokuwa wanacheza kwenye Club zao waliko tokea

Hayo maneno yalisemwa na nyinyi mashabiki

Na hii ni kawaida, ipo hata kwa Simba, kitu nachokiona hapa ni kwamba nyinyi mashabiki ni kama ndio mna uhalali wa kuisema timu yenu vile mtakavyo, ila maneno hayo yakisemwa na mchambuzi tayari inakuwa nongwa, mchambuzi fulani ana chuki

Mimi napenda kusikiliza Dunia ya michezo wapo Radio, pale kuna mchambuzi anaitwa Salumu Mnolela, yule anasema kabisa kuwa Simba mbovu na anakupa na sababu. Simba haina kikosi kipana, Quality ya mchezaji mmoja mmoja bado ni tatizo na mimi namkubalia na pia nakumkubali kama mchambuzi mzuri.

Wala sioni kama hiyo ni chuki kwasababu anachokiongea kinaonekana, so siwezi kutafuta kimechi kimoja kama kile cha Mtibwa nikashinda goli 5 afu nikakitumia hicho kuanza kumsema Salum Mnolela kuwa ni mnafki anachuki na Simba kwasababu kikosi alichosema kibovu kimeshinda bao 5.

Maoni ya wachambuzi yaheshimiwe japo hayawezi kuwa sahihi ila please tusiwajengee chuki. Tutawafanya wawe wanalazimika kuongea unafki ili tu kuturidhisha mashabiki.
 
Mnajotekenya na kucheka wenyewe

Yani hata hii mechi ya mzee wa tozo na bahasha unataka kuisifu yanga?

Kiufupi jana yanga lichezapeke yake mengine yote mwigulu madelu syatem nchemba kashamaliza

Sent from my M100 using JamiiForums mobile app
 
Mnajotekenya na kucheka wenyewe

Yani hata hii mechi ya mzee wa tozo na bahasha unataka kuisifu yanga?

Kiufupi jana yanga lichezapeke yake mengine yote mwigulu madelu syatem nchemba kashamaliza

Sent from my M100 using JamiiForums mobile app
Nyie mlipocheza na mtibwa yenye upungufu wa wachezaji 2 ilikuwa ni bahasha ya bei gani mkuu, mkishinda nyie ni halali akishinda yanga ni bahasha, kweli mbumbumbu mnateseka na mtateseka sana tu
 
I second you. Bravo Brother
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…