Wachambuzi wa Crown Sports, Hans Raphael na Geoff Lea wanabishana kama wanagombana wakiwa live kwenye kipindi

ESCORT 1

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2015
Posts
1,412
Reaction score
3,043
Nasikiliza hapa Crown Sports ya Crown FM, wachambuzi wa kipindi hiko wanajadili ile faulo iliyozaa goli la Simba.

Hans anasema sio goli halali kwakuwa mpira ulianzishwa katika eneo sio sahihi kwakuwa ulisogezwa.

Geoff Lea anasema goli ni halali kwakuwa sio lazma mpira uanzishwe eneo lile lile.

Basi wakaanza kubishana kwa virugu huku kipindi kikiwa live. Tatizo kuu Hans Raphael huwa hawapi nafasi wenzake kila saa anataka kuongea yeye.

Mwisho wa siku, Hans akamuambia Geoff kuwa ujue tupo live, Geoff akamjibu kwahyo sisi tunaongea pumba na wewe pekee yako ndio unaongea point!!

Hii imekaaje kitaaluma?
 
Hivi media zote hazina vipindi vingine zaidi ya michezo?

Yani asubuhi yote hii hadi jioni mpaka usiku ni michezo tu,

Alafu mnataka Marekani iendelee kutupa hela zake wakati sisi muda wote tunajadili simba na yanga?
 
Ndio vyepesi na vina Hela na wasikilizaji wengi

NB : Tanzania naoaga kila mtu mchambuzi awe wa Soka au Siasa
 
Bado tu kuna watu wanasikilizaga redio.?

ADA11642-6832-4CAD-A6AB-5D096C55AF28.jpeg
 
Jemedari Said, Leah na Hans ni watu wasiopenda kushindwa, wakikosolewa ni kosa!
Wana content nzuri, nafikiri wakiweka utaratibu mzuri wa namna ya kujadili hoja zao kipindi kitanoga.

Hans kipindi yuko Wasaf alikuwa muelewa sana, akishatoa hoja yake anakaa zake kimya.

Kama sio marketing strategy ya Crown, wanahitaji kuchukua hatua.
 
Kwani anaesimamia kipindi ni nani,anatakiwa kusimamia hilo

Clouds ndo walianzisha huu utaratibu wa kipindi kimoja kuwa na watangazaj zaidi ya wawili na wamejitahid sana kuachiana nafas za kuzungumza lakin wasafi kuna wakat huwa ni kelele

Clouds walipata shida sana kwa Mwijaku na Mchomvu
 
Nasikiliza hapa Crown Sports ya Crown FM, wachambuzi wa kipindi hiko wanajadili ile faulo iliyozaa goli la Simba.

Hans anasema sio goli halali kwakuwa mpira ulianzishwa katika eneo sio sahihi kwakuwa ulisogezwa.

Geoff Lea anasema goli ni halali kwakuwa sio lazma mpira uanzishwe eneo lile lile.

Basi wakaanza kubishana kwa virugu huku kipindi kikiwa live. Tatizo kuu Hans Raphael huwa hawapi nafasi wenzake kila saa anataka kuongea yeye.

Mwisho wa siku, Hans akamuambia Geoff kuwa ujue tupo live, Geoff akamjibu kwahyo sisi tunaongea pumba na wewe pekee yako ndio unaongea point!!

Hii imekaaje kitaaluma?
Weka video nione kidogo timbwili lilivyokuwa
 
Wangepigana sasa ila mbishi zaidi ni Job George

Kwani anaesimamia kipindi ni nani,anatakiwa kusimamia hilo

Clouds ndo walianzisha huu utaratibu wa kipindi kimoja kuwa na watangazaj zaidi ya wawili na wamejitahid sana kuachiana nafas za kuzungumza lakin wasafi kuna wakat huwa ni kelele

Clouds walipata shida sana kwa Mwijaku na Mchomvu
Kwani mwijaku utangazaji kasomea ama
 
Bora hao unajua kabisa hawa wana bishania kitu gani kuna wale wa wasafi sijui kipindi gani kile.....

Mtangazaji no 1: Tanzaniaa
Mtangazaji no 2: Umesemajeee
Mtangazaji no 1: Tanzaniaaaaaaaaaa!
Mtangazaji no 2: umesema Tanzaniaa
Mtangazaji no 1: Yan Tanzaniaaaaaaaaa!

Nazimaga redio nakonect Device and read to pair
 
Back
Top Bottom