Wachambuzi wa Crown Sports, Hans Raphael na Geoff Lea wanabishana kama wanagombana wakiwa live kwenye kipindi

Nasikiliza hapa Crown Sports ya Crown FM, wachambuzi wa kipindi hiko wanajadili ile faulo iliyozaa goli la Simba.

Hans anasema sio goli halali kwakuwa mpira ulianzishwa katika eneo sio sahihi kwakuwa ulisogezwa.

Geoff Lea anasema goli ni halali kwakuwa sio lazma mpira uanzishwe eneo lile lile.

Basi wakaanza kubishana kwa virugu huku kipindi kikiwa live. Tatizo kuu Hans Raphael huwa hawapi nafasi wenzake kila saa anataka kuongea yeye.

Mwisho wa siku, Hans akamuambia Geoff kuwa ujue tupo live, Geoff akamjibu kwahyo sisi tunaongea pumba na wewe pekee yako ndio unaongea point!!

Hii imekaaje kitaaluma?
Hans = Maziwa

Geof Lea = BANGI

HAWAWEZI KUELEWANA.
 
Hans ni mtu wa kukurupuka muda wote na mpenda ubishi hata kama amezidiwa kwa hoja
Anahikubali na kujifanya kuujua sana mpira ndio maana mara nyingi amekuwa akibishana na kina Jemedari na Geoff ambao kimsingi wamemuacha mbali kiuchambuzi anapaswa kujifunza kwao
 
Hivi media zote hazina vipindi vingine zaidi ya michezo?

Yani asubuhi yote hii hadi jioni mpaka usiku ni michezo tu,

Alafu mnataka Marekani iendelee kutupa hela zake wakati sisi muda wote tunajadili simba na yanga?
Ni kweli Kawaida michezo inatakiwa kufanyika/kuchezwa hata kujadiliwa baada ya shughuli zoote za uzalishaji mali...ndio maana mechi huchezwa jioni au usiku popote duniani..

Na Sio kila Siku, michezo hufanyika mostly weekend.....
Culture ya kuiweka michezo ifanyike baada ya kazi nyingine ni universal..na haijafanywa kwa bahati mbaya..

Na ndio maana hata kwny Magazeti au television, habari za michezo huwekwa mwishoni baada ya taarifa zote...popote duniani utaratibu ndio huo.

Sasa ukiona Taifa ambalo raia wake wanaamkia kujadili michezo 24/7 ujue sio Kiashiria kizuri.

Media haziwezi kulaumiwa direct kwasab pengine wao ndio wameona content ya michezo ndio inayouza zaidi....lakini shida ipo kwny hiyo jamii.
 
Huyo Hans Rafael Mwombeki ndo muasisi wa maneno kama low block, high pressing, double pivot, high line, false number nine, inverted winger na mengine mengi sana ndo yaliyomwingiza mjini kwenye ulimwengu wa wachambuzi akianzia pale wasafi FM na mwenzie Nasri Khalfan. Kwakifupi dogo ni mbishi afu ni mtoto wa elfu 2000 kaukuta mpira kwenye teknolojia ya juu sana na ndo kinachomsaidia. Kujilinganisha na Geof Lea ni uongo kwasababu huyo jamaa ni kale kamwili kake tu ila ni mkongwe Mimi nimeanza kumskia around 2008/9 wakichambua mpira kwenye kipindi cha sports extra ya Clouds FM na akina Shaffih Dauda, Edo Kumwembe, Ibrahim Masoud Maestro na lile bonanza lao sijui lilikua linaitwaje wanagawana timu za Ulaya afu wanashindana, kitambo sana na hapo miaka hiyo ndo tumemaliza advance tunajiandaa kwenda chuo, sasa huyu bwana mdogo sijui alikua wapi. Kwa Jemedari ndo kabsaa maana kwanza jamaa mpira aliucheza tena kwenye kiwango kikubwa tu hadi premier league. Anyways cha msingi dogo anakuja vizuri, anaufuatilia mpira vizuri na ni mbunifu sana tatizo ubishi na ujuaji hataki kujifunza kwa wenzake.
 
Angalau ndo vipindi ambavyo viko real kiasi, Hivyo vingine ni mapambia ya kusifu na kuabudu Mama mama mama
 
Hivi media zote hazina vipindi vingine zaidi ya michezo?

Yani asubuhi yote hii hadi jioni mpaka usiku ni michezo tu,

Alafu mnataka Marekani iendelee kutupa hela zake wakati sisi muda wote tunajadili simba na yanga?
Ndo kwenye hela huoni makampuni ya kubeti yanashindana kwa matangazo na vijana wakifanya beti na michezo kama ajira rasmi.
 
Ni kweli Kawaida michezo inatakiwa kufanyika/kuchezwa hata kujadiliwa baada ya shughuli zoote za uzalishaji mali...ndio maana mechi huchezwa jioni au usiku popote duniani..

Na Sio kila Siku, michezo hufanyika mostly weekend.....
Culture ya kuiweka michezo ifanyike baada ya kazi nyingine ni universal..na haijafanywa kwa bahati mbaya..

Na ndio maana hata kwny Magazeti au television, habari za michezo huwekwa mwishoni baada ya taarifa zote...popote duniani utaratibu ndio huo.

Sasa ukiona Taifa ambalo raia wake wanaamkia kujadili michezo 24/7 ujue sio Kiashiria kizuri.

Media haziwezi kulaumiwa direct kwasab pengine wao ndio wameona content ya michezo ndio inayouza zaidi....lakini shida ipo kwny hiyo jamii.
Serikali isiyopenda kuwajibika na bugudha ndo inapenda ili iendelee kutawala kwa uzalendo wakati huo watanzania tunakoksa na petty ishu😁
 
Huyo Hans Rafael Mwombeki ndo muasisi wa maneno kama low block, high pressing, double pivot, high line, false number nine, inverted winger na mengine mengi sana ndo yaliyomwingiza mjini kwenye ulimwengu wa wachambuzi akianzia pale wasafi FM na mwenzie Nasri Khalfan. Kwakifupi dogo ni mbishi afu ni mtoto wa elfu 2000 kaukuta mpira kwenye teknolojia ya juu sana na ndo kinachomsaidia. Kujilinganisha na Geof Lea ni uongo kwasababu huyo jamaa ni kale kamwili kake tu ila ni mkongwe Mimi nimeanza kumskia around 2008/9 wakichambua mpira kwenye kipindi cha sports extra ya Clouds FM na akina Shaffih Dauda, Edo Kumwembe, Ibrahim Masoud Maestro na lile bonanza lao sijui lilikua linaitwaje wanagawana timu za Ulaya afu wanashindana, kitambo sana na hapo miaka hiyo ndo tumemaliza advance tunajiandaa kwenda chuo, sasa huyu bwana mdogo sijui alikua wapi. Kwa Jemedari ndo kabsaa maana kwanza jamaa mpira aliucheza tena kwenye kiwango kikubwa tu hadi premier league. Anyways cha msingi dogo anakuja vizuri, anaufuatilia mpira vizuri na ni mbunifu sana tatizo ubishi na ujuaji hataki kujifunza kwa wenzake.
Geoffrey Lea kamaliza form six 2006 pale Green Acres Sala sala
 
Back
Top Bottom