Yaani nawe unatumia muda wako kumchukulia serious Laban og kama mchambuzi? Huyo anatumia hili jukwaa la michezo kama sehemu ya kujifurahisha na ndio maana unaona nyuzi zake zimejaa kuisifia Yanga na kuiponda Simba pekee. Ukichukua takwimu ya Azam vs Yanga na Azam vs Simba, unaona nafasi ya Azam kuifunga Simba ni bahati nasibu maana wanaongoza kwa kufungwa na Simba. Huwa wanaonesha ushindani dhidi ya Yanga na huumia sana wakifungwa na Yanga ila sio Simba. Jana wachezaji wa Azam na kiongozi wao walikuwa wapo na furaha tu huku wakipigiwa makofi. Ngoja uone mechi ya Yanga Akamiko atajipanga hadi amvunje mtu.