Wachambuzi wa Mpira katika Redio za Tanzania tutaanza Kuwadharau sasa, Goli la Yanga SC lilikuwa halali kwa Uzembe wa Kipa

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
8,018
Reaction score
16,802
Mimi ni Shabiki wa Simba SC ila kwa Upuuzi wenu huu wa Kuchambua Kiuwoga au Kimahaba au kwa Bahasha Kunawaharibia na wenye Akili, tusio Wanafiki na wapenda Haki sasa tutaanza Kuwadharau na hata Kutosikiliza hivyo Vipindi vyenu vya Michezo vya Redio.

Halafu nyie Wachambuzi wa Michezo katika Redio mbalimbali za Tanzania tambueni wengine mnaotudanganya siyo tu tunaujua huo Mpira bali pia tumeshaucheza mno na wengine huenda isingekuwa ni Mikwara ya Wazazi Wetu Wanoko kututaka tujikite katika Elimu leo tungekuwa hata PSG tunaupiga mwingi huko.

Hivi nyie Wachambuzi wa Michezo katika Redio mbalimbali nchini mmepata wapi Uhalali wa kusema kuwa lile Goli alilofunga Fiston Mayele ni Offside ( Kaotea ) wakati amefunga Kihalali kwa Uzembe wa Goalkeeping Principles ambapo Kipa Mwenyewe ndiyo alishindwa Kuudaka ipasavyo Mpira na ukamponyoka na Mayele Kufunga?

Haya Wachambuzi mlioanza Kukosea kwa Usiku huu ni wa Clouds FM akina Nicas Kotinyo ( mwana Simba SC Mwenzangu ), Privaldinho na Edgar Kibwana ( wana Yanga SC ) hivyo nawaomba Wachambuzi wengine wa Vipindi vya Michezo vya Kesho Asubuhi, Mchana na Jioni vya Kesho nanyi msirudie Upuuzi huu na semeni Ukweli bila Unafiki, Uwoga na Kupepesa kama Mimi Mightier kuwa Goli like kwa 100% lilikuwa ni halali ila sema tu Mwamuzi ( Referee ) aliamua Kuwanyima / Kuwakatalia Yanga SC.

Tuwe Wanamichezo na siyo Mashabiki!!
 
Wachambuzi wa hovyo kabisa, Mimi walinishangaza wachambuzi wa Azam Sports 1, kipindi Cha mapumziko, kutokuongelea utata uliopo dhidi ya zile offside za dhulma, yaani sijui wanaogopa Nini! Wajifunze basi ata kwa wenzao wa ulaya, utata Kama ule uwa unaongelewa kwa kwa undani zaidi ikiongozwa na utoaji wa Elimu.

Ila wa huku bongo sijui ni nini yaani, maoga mno ata kuongelea, wakati Ile ni tasnia yao, yawapasa kuongea kwa uwazi zaidi na hata kurumbana kwa hoja, ila mioga mno michambuzi ya huku, wanaboa!!
 
Nimeshangaa pia. Mpira kaugusa kipa akabaki last opponent kama ilivokua kwa Kagere dhidi ya Mbeya kwanza. Kwa nn Mayele ahukumiwe offside? Double Standards?
 
Mimi ni Shabiki wa Simba SC ila kwa Upuuzi wenu huu wa Kuchambua Kiuwoga au Kimahaba au kwa Bahasha Kunawaharibia na wenye Akili, tusio Wanafiki na wapenda Haki sasa tutaanza Kuwadharau na hata Kutosikiliza hivyo Vipindi vyenu vya Michezo vya Redio...
Lilikuwa halali kwa sheria ipi?hivi hata sheria za mpira unazijua kwel ww?

Au unachukulia mazoea tu?

Kasome sheria then urudi hapa
 
Nami nasubiri jibu.

Kama mpira ulitoka kwa kipa ni goli. Ila kama ulitoka kwa mchezaji wa yanga sio goli ni offside.
 
Mkuu..

Mpira aliopiga Mayele ulitoka kwa nani?
Baada ya Golikipa "kuutema" ule mpira, ulianguka kwa Yannick Bangala.
Bangala alimpa pasi (assist) Fiston Mayele ambaye alikua kwenye eneo la kuotea.

Hivyo incidence ile ni offside.

Kwa sababu binadamu tumeumbiwa kusahau, teknolojia ina tabia ya kutukumbusha.

Tazama hapa...

Mkuu acha kutudanganya, wakati Bangala anapiga pasi kwenda kwa Mayele, haumuoni beki wa biashara akiwa yupo golini? Mayele kapokea pasi akiwa onside position. Rudia hiyo video kutazama halafu angalia position aliyosima mayele vs position aliyokuwepo beki wa Biashara halafu niambie nani alikuwa mbele ya mwenzie
 
Mimi ni Shabiki wa Simba SC ila kwa Upuuzi wenu huu wa Kuchambua Kiuwoga au Kimahaba au kwa Bahasha Kunawaharibia na wenye Akili, tusio Wanafiki na wapenda Haki sasa tutaanza Kuwadharau na hata Kutosikiliza hivyo Vipindi vyenu vya Michezo vya Redio.

Halafu nyie Wachambuzi wa Michezo katika Redio mbalimbali za Tanzania tambueni wengine mnaotudanganya siyo tu tunaujua huo Mpira bali pia tumeshaucheza mno na wengine huenda isingekuwa ni Mikwara ya Wazazi Wetu Wanoko kututaka tujikite katika Elimu leo tungekuwa hata PSG tunaupiga mwingi huko.

Hivi nyie Wachambuzi wa Michezo katika Redio mbalimbali nchini mmepata wapi Uhalali wa kusema kuwa lile Goli alilofunga Fiston Mayele ni Offside ( Kaotea ) wakati amefunga Kihalali kwa Uzembe wa Goalkeeping Principles ambapo Kipa Mwenyewe ndiyo alishindwa Kuudaka ipasavyo Mpira na ukamponyoka na Mayele Kufunga?

Haya Wachambuzi mlioanza Kukosea kwa Usiku huu ni wa Clouds FM akina Nicas Kotinyo ( mwana Simba SC Mwenzangu ), Privaldinho na Edgar Kibwana ( wana Yanga SC ) hivyo nawaomba Wachambuzi wengine wa Vipindi vya Michezo vya Kesho Asubuhi, Mchana na Jioni vya Kesho nanyi msirudie Upuuzi huu na semeni Ukweli bila Unafiki, Uwoga na Kupepesa kama Mimi Mightier kuwa Goli like kwa 100% lilikuwa ni halali ila sema tu Mwamuzi ( Referee ) aliamua Kuwanyima / Kuwakatalia Yanga SC.

Tuwe Wanamichezo na siyo Mashabiki!!
Mkuu, kwanini kwenye clear offside incidence wewe umeamua kusema ni goli halali ?

Ule mpira umeguswa na watu watano.
(1) Saido - Yanga alipiga kona kwenda kwa (2.) Aucho - Yanga.
Aucho "akamwaga maji" (3) Ssetuba - Biashara "akasev", mpira ukaanguka kwa (4) Bangala, na hatimaye Bangala akatoa pasi kwa (5) Mayele - Yanga, ambaye alifunga goli.

Saidi .... Aucho ... Ssetuba ... Bangala... Mayele.

Ruling ya offside, unaitazama kutoka kwa "Bangala kwenda kwa Mayele",
Kama Bangala alimpa pasi Mayele akiwa kwenye eneo la kuotea, basi hiyo ni offside bila kujalisha Ssetuba, Aucho au Saido walifanya nini.

Nimeona hoja yako umeijenga kwenye suala la Ssetuba kugusa mpira.

Kwanini Mayele alikua offside:
Alikua offside kwa sababu wakati Bangala anampa pasi, mbele yake kulikua na mchezaji mmoja tu wa Biashara United badala ya angalau wachezaji wawili. (Wachezaji hao sio lazima mmoja wao awe golikipa).

NB: Natamani sana kujifunza, ni kwanini unesema hii haikua offside kwa mujibu wako. Elimu ni bahari, niko tayari kujifunza toka kwako mkuu.

Nimeshangaa pia. Mpira kaugusa kipa akabaki last opponent kama ilivokua kwa Kagere dhidi ya Mbeya kwanza. Kwa nn Mayele ahukumiwe offside? Double Standards?
Ile ni offside brother! Usembe ni wa kipa kweli lakini yule uliyemfikia hakupaswa kutoa pass angepiga direct isingekuwa offside ila alipotoa pasi ilitafsiliwa kuwa aliepokea pass alikuwa amebaki na mtu mmoja kulifikia lango na kwa mujibu wa sheria za soka ikiwa iko hivo ni offside haijalishi pale gorini kuna kipa au beki
 
Mkuu acha kutudanganya, wakati Bangala anapiga pasi kwenda kwa Mayele, haumuoni beki wa biashara akiwa yupo golini? Mayele kapokea pasi akiwa onside position. Rudia hiyo video kutazama halafu angalia position aliyosima mayele vs position aliyokuwepo beki wa Biashara halafu niambie nani alikuwa mbele ya mwenzie
Rule ya offside inasema hivi:

Itakua ni offside pale ambapo mchezaji anayeshambulia (Mayele) atapokea pasi kutoka kwa mchezaji mwenzake (Bangala) huku mbele yake kukiwa mchezaji mmoja wa timu inayozuia (sio lazima awe golikipa).
Ili isiwe offside, ni lazima mbele ya mfungaji kuwe na angalau wachezaji wawili wa timu inayozuia.

Mtu pekee ambaye alikua mbele ya Mayele alikua ni Beki wa biashara ambaye alikua golini, na hii umesema mwenyewe, sasa kwanini unabisha kwamba sio offside mkuu ?

Kwa kupanua ufahamu, iko hivi;
Offside inapimwa kutoka alipo mlinzi wa pili kutoka mwisho. Kama golikipa akiwa golini, anakua ni mlinzi wa kwanza, mlinzi wa pili atakua ni mchezaji yeyote wa timu ya golikipa huyo aliye karibu na mlinzi wa kwanza.
Kwahiyo chora mstari kutoka kwa Mayele na mlinzi wa pili kutoka mwisho na sio mlinzi wa mwisho (beki aliyekuwapo golini).

Vinginevyo labda mwenzetu uamue kutumia sheria za Tennis, Golf au Karata kuhalalisha hili.
 
Mimi nadhani aliyepigiwa offside ni Moloko si mayele na kisheria ikishaamuliwa basi matendo mengine yanayofuata yanakuwa yamekatishwa na kusitishwa uhalali wake rasmi

Tazama wakati mpira unakuja Moloko alikuwa wapi
 
Rule ya offside inasema hivi:

Itakua ni offside pale ambapo mchezaji anayeshambulia (Mayele) atapokea pasi kutoka kwa mchezaji mwenzake (Bangala) huku mbele yake kukiwa mchezaji mmoja wa timu inayozuia (sio lazima awe golikipa).
Ili isiwe offside, ni lazima mbele ya mfungaji kuwe na angalau wachezaji wawili wa timu inayozuia.

Mtu pekee ambaye alikua mbele ya Mayele alikua ni Beki wa biashara ambaye alikua golini, na hii umesema mwenyewe, sasa kwanini unabisha kwamba sio offside mkuu ?

Kwa kupanua ufahamu, iko hivi;
Offside inapimwa kutoka alipo mlinzi wa pili kutoka mwisho. Kama golikipa akiwa golini, anakua ni mlinzi wa kwanza, mlinzi wa pili atakua ni mchezaji yeyote wa timu ya golikipa huyo aliye karibu na mlinzi wa kwanza.
Kwahiyo chora mstari kutoka kwa Mayele na mlinzi wa pili kutoka mwisho na sio mlinzi wa mwisho (beki aliyekuwapo golini).

Vinginevyo labda mwenzetu uamue kutumia sheria za Tennis, Golf au Karata kuhalalisha hili.

Kiukweli ni kiri tu kuwa hili nilikuwa silijui. Nilijua kipa anapotoka anakuwa anahesabiwa kama mmoja wapo wa timu inayozuia. Hivyo beki na kipa kufanya idadi ya wawili. Ila nashukuru umenifanya nilifatilie hili na nimejiridhisha pasi na shaka kuwa ni clear offside. Jamani tusiojua hili tupitie hii kuna hadi mifano ya hili sheria ya offside kipa anapokuwa katoka.
 
Mimi ni Shabiki wa Simba SC ila kwa Upuuzi wenu huu wa Kuchambua Kiuwoga au Kimahaba au kwa Bahasha Kunawaharibia na wenye Akili, tusio Wanafiki na wapenda Haki sasa tutaanza Kuwadharau na hata Kutosikiliza hivyo Vipindi vyenu vya Michezo vya Redio.

Halafu nyie Wachambuzi wa Michezo katika Redio mbalimbali za Tanzania tambueni wengine mnaotudanganya siyo tu tunaujua huo Mpira bali pia tumeshaucheza mno na wengine huenda isingekuwa ni Mikwara ya Wazazi Wetu Wanoko kututaka tujikite katika Elimu leo tungekuwa hata PSG tunaupiga mwingi huko.

Hivi nyie Wachambuzi wa Michezo katika Redio mbalimbali nchini mmepata wapi Uhalali wa kusema kuwa lile Goli alilofunga Fiston Mayele ni Offside ( Kaotea ) wakati amefunga Kihalali kwa Uzembe wa Goalkeeping Principles ambapo Kipa Mwenyewe ndiyo alishindwa Kuudaka ipasavyo Mpira na ukamponyoka na Mayele Kufunga?

Haya Wachambuzi mlioanza Kukosea kwa Usiku huu ni wa Clouds FM akina Nicas Kotinyo ( mwana Simba SC Mwenzangu ), Privaldinho na Edgar Kibwana ( wana Yanga SC ) hivyo nawaomba Wachambuzi wengine wa Vipindi vya Michezo vya Kesho Asubuhi, Mchana na Jioni vya Kesho nanyi msirudie Upuuzi huu na semeni Ukweli bila Unafiki, Uwoga na Kupepesa kama Mimi Mightier kuwa Goli like kwa 100% lilikuwa ni halali ila sema tu Mwamuzi ( Referee ) aliamua Kuwanyima / Kuwakatalia Yanga SC.

Tuwe Wanamichezo na siyo Mashabiki!!
Mkuu pale unapozitafuta kick kutoka utopolo.... we noma sana..uto wameomba wenyewe sheria 17 zifanye kazi..na ndo zimeanza bahati mbaya mafamba kama nyie mnakaa humu kupotosha potosha tuuu.... idiot
 
Nadhani wamelogwa nao

Nimerudia ile clip mara 4 aliyekuwa offside position alikuwa moloko lkn hakunufaika na mpira golikipa alipopangua ukamgonga mchezaji baadaye yanga wakaanza pasi na mayele akafunga akiwa hakuotea

Sent from my Nokia C1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom