Wachambuzi wetu wa soka badilikeni!

MTAZAMO

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2011
Posts
19,675
Reaction score
33,583
Wakuu,

Siku za karibuni nchi yetu imeshuhudia industry mpya ya uchambuzi ya soka ambayo imejizolea umaarufu mkubwa na kutengeneza ajira za vijana wengi.

Pamoja na kuwa na wachambuzi wengi hivi sasa lakini wanafanana mambo mengi sana labda ndani yao waibuke watu watakaokuja kujitofautisha na kuongeza u serious kidogo.

Hapa nitatoa mifano michache ya makosa yao hao ambao wamejiajiri huko na kupaswa kufanya mambo kwa weledi zaidi kuliko mashabiki.

Mfano nimegusia mambo mawili tu ...

1) Upashanaji wa habari mpya
Hapa lipo tatizo kubwa, wapo ambao wanatupa habari za ndani kabla hazijawa rasmi sina tatizo hapo. Lakini tatizo lipo habari inapotoka rasmi jinsi wachambuzi wetu wanavyoi report.

Mfano mdogo ni leo ambapo Simba wamemtangaza kocha mpya, wachambuzi wote wamepost hiyo taarifa! Hivi ni shabiki gani haja follow account ya Simba au vyombo vya habari maarufu vyenye wajibu wa kutuhabarisha? Kila mchambuzi unayekimbilia page yake amepost hiyo taarifa bila any analysis.

Wachambuzi wengi habari kama hii ya huyu kocha mpya walishaijua siku chache iliyopita hivyo tulitegemea waje na taarifa za kutosha na uchambuzi kuhusu kocha huyu ikiwemo falsafa ya soka lake maana kila kitu kipo wazi. Lakini wachambuzi wote wamegeuka Millard Ayo na ukiona yupo aliye post analysis wata repost hiyo hiyo! Alafu tutaulizwa ni Big Yes or No [emoji41]

2) Uchambuzi wa soka
Hapa nisingependa kwenda ndani sana lakini yapo machache, mfano Simba ilipokuwa inaenda kucheza na ile timu ya Nigeria au hata FC Platinum, wachambuzi wengi walikosa cha kuchambua kwa kizingizio kutozijua hizo timu! Kweli ktk ulimwengu huu wa leo ambao ni kijiji?

Pia linapoibuka sakata ambalo ni la kisheria za soka tu inakuwa aibu namna wanavyotolea maelezo na mfano mzuri ni sakata la Bernard Morrison au issue ya Simba na FFC. Wachambuzi ndio walipaswa kuibua mambo kwenye angle ambayo mashabiki na wadau wengine hatuoni lakini nao wanaishia kujadiliana kwenye vipindi blindly kama ilivyo kwenye vijiwe vyetu tu na hakuna jipya.

Wachambuzi wengi wanajitahidi maeneo mengi hasa analysis ya mpira waliouona lakini kuna vitu vingi sana hawajiongezi na kujikuta wana vitrend vinavyofanana sana.

Kwasasa mmefanikiwa kutengeneza nafasi yenu kwenye industry basi jitahidini kuongeza thamani kabla wadau hawajarudi kutumia watangazaji wa michezo kama ilivyokuwa zamani ambao wanaweza kuuza chai kidogo [emoji41]

Nyie mna vipaji na mmejikita huko kama wachambuzi, fanyeni analysis za mambo kwa undani badala ya kuwa na ufahamu kama sisi mashabiki.

Endeleeni na kazi nzuri na mjiongeze kidogo kulinda kiwanda chenu.
 
kama umeona gap in the market jitose tu anza kuchambua huenda ukawapa changamoto wakabadilika to the better
 
kama umeona gap in the market jitose tu anza kuchambua huenda ukawapa changamoto wakabadilika to the better
Sisi tuliogonga 40s tunaogopa ku switch carrier lakini kuna gap kubwa sana. Imagine uwe na mchambuzi mwenye kariba ya Zitto kwenye kupenda kusoma na ku analyse? Nafikiri wengi wamefata mikumbo ya waliopo badala ya kujitengenezea utofauti.

Ally Mayai hana followers wengi lakini angekuwa active mitandaoni level ya Shaffih au Edo angetoa changamoto walau.
 
Mimi nina mtizamo tafauti kwenye hili game ambalo ni subjective na jambo moja huenda watu wasikubaliane (nane amesema /who is talking) ina matter sana tena sana.., ndio maana kama hawa wachezaji wanaoretire wakiingia katika kuchambua soka huenda wakasikilizwa zaidi hata kama wanaongea pumba (implication kwamba wanajua wanachokiongea) kwahio hili suala sio kwenye soka tu, siku hizi wengi wanaongea vapour tu mtu anaingia wikipedia research ya dakika mbili anaanza ku-recycle materials
 
Yaaani hongera sana kwa kuona ombwe hili la hawa wanaojiita wachambuzi. Juzi hapa kuna mchambuzi anajiita Edo. Anaongelea suala la Chikwembe either kucheza CAF championship au kutokucheza, Ameshindwa hata kutafuta kanuni za hayo mashindano ili anatoa maelezo sahihi. Yeye anaenda kutoa mfano wa mashindano ya UEFA , na wakati huo huo sheria anayoitolea mfano ilisharekebishwa mwaka juzi na msimu uliopita waliitumia. Sisi hatuna Wachambuzi wa soka ila tuna watoa maelezo kwa matukio yaliojitokeza. Kidogo Ambagile huwa ana jitahidi kama jambo hana uhakika nalo anasema kabisa kua ngoja atafute ukweli wa jambo yenyewe
 
Mara nyingi tunakimbilia kwao kupata facts alafu unakuta chai tu [emoji41]
 
Wachambuzi wa bongo wengi ni vishoka tu kama walikomaa na Busha la Morrison ila sasa hivi hawawezi hata kuongea tena Baada ya kumuona anafanya mazoezi kule bunju na hapo ndio ninaamini wengi wa wachambuzi huokota habari pasipo kuzikuzichambua
 
Bongo hakuna wachambuzi. hakuna tofauti yao na sisi tunaopost humu.wanakimbizana kuwa wa kwanza kupost. Mwingine anaitwa Oscar huko insta amechagua kuwa comedian mpuuzi

 
Kuna kipuuzi kinajiita privadinho ni kibishi sana kina kiherehere mnooo ila nimweupe sanaa
 
Pamoja na mtoa thread kuonekana ume elemea kwenye ushabiki wa simba au mambo yaliyo itokea simba, bado nakupa heshima kubwa ya jicho lako pevu. Kumekuwa na ongezeko kubwa la sports pundits bahati mbaya wana chambua kwa hisia kuliko maarifa, hii ni ajenda kubwa mno na ina hitaji mjadala wa kitaifa tena uendeshwe na wizara ya habari. ASANTE KWA KULIONA HILI
 
Kuna dogo anaitwa Farhan_jr anajua kufanya analysis vizuri, Edo na Shaffih si wazuri sana katika analysis ila ukongwe unawabeba, George Ambangile yupo vizuri sana ila tatizo anapenda kuplay safe sana na kujikita katika soka la Ulaya zaidi na la Bongo kulipotezea kitu ambacho anashindwa kuelewa siku hizi habari za Simba na Yanga zipo hot kushinda hizo club za Ulaya na zinafuatiliwa sana. Yupo Privaldinho anajituma sana kutafuta habari exclusive
 

Siku moja George aliulizwa atoe maoni yake kuhusu issue ambayo ilikuwa related na sheria, akajibu kwamba hana maoni kwa sababu hana uelewa na hilo swala, kwa hiyo isije akanukuliwa kwa kitu asichokijua vizuri.

Baada ya kujibu hivyo mtangazaji akaendelea kumlazimisha atoe tu mtazamo wake, jamaa akasisitiza kwamba hawezi.

Hilo lilikuwa jibu zuri sana, ila wengine ndo hapo wangebumba maoni halafu kuna wasikilizaji wangeyabeba kama yalivyo.
 
Ambangile yupo vizuri sana kichwani laiti angetumia page zake za mitandao ya kijamii kuanalyse mechi za nyumbani kama ilivyo za Ulaya tungepata unbiased analysis bora zaidi kuliko hata yale mambo 10 ya Ali Kamwe.
 
Basi mna moyo hata wa kuwafollow hao wacha-mbuzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…