MTAZAMO
JF-Expert Member
- Feb 8, 2011
- 19,675
- 33,583
Wakuu,
Siku za karibuni nchi yetu imeshuhudia industry mpya ya uchambuzi ya soka ambayo imejizolea umaarufu mkubwa na kutengeneza ajira za vijana wengi.
Pamoja na kuwa na wachambuzi wengi hivi sasa lakini wanafanana mambo mengi sana labda ndani yao waibuke watu watakaokuja kujitofautisha na kuongeza u serious kidogo.
Hapa nitatoa mifano michache ya makosa yao hao ambao wamejiajiri huko na kupaswa kufanya mambo kwa weledi zaidi kuliko mashabiki.
Mfano nimegusia mambo mawili tu ...
1) Upashanaji wa habari mpya
Hapa lipo tatizo kubwa, wapo ambao wanatupa habari za ndani kabla hazijawa rasmi sina tatizo hapo. Lakini tatizo lipo habari inapotoka rasmi jinsi wachambuzi wetu wanavyoi report.
Mfano mdogo ni leo ambapo Simba wamemtangaza kocha mpya, wachambuzi wote wamepost hiyo taarifa! Hivi ni shabiki gani haja follow account ya Simba au vyombo vya habari maarufu vyenye wajibu wa kutuhabarisha? Kila mchambuzi unayekimbilia page yake amepost hiyo taarifa bila any analysis.
Wachambuzi wengi habari kama hii ya huyu kocha mpya walishaijua siku chache iliyopita hivyo tulitegemea waje na taarifa za kutosha na uchambuzi kuhusu kocha huyu ikiwemo falsafa ya soka lake maana kila kitu kipo wazi. Lakini wachambuzi wote wamegeuka Millard Ayo na ukiona yupo aliye post analysis wata repost hiyo hiyo! Alafu tutaulizwa ni Big Yes or No [emoji41]
2) Uchambuzi wa soka
Hapa nisingependa kwenda ndani sana lakini yapo machache, mfano Simba ilipokuwa inaenda kucheza na ile timu ya Nigeria au hata FC Platinum, wachambuzi wengi walikosa cha kuchambua kwa kizingizio kutozijua hizo timu! Kweli ktk ulimwengu huu wa leo ambao ni kijiji?
Pia linapoibuka sakata ambalo ni la kisheria za soka tu inakuwa aibu namna wanavyotolea maelezo na mfano mzuri ni sakata la Bernard Morrison au issue ya Simba na FFC. Wachambuzi ndio walipaswa kuibua mambo kwenye angle ambayo mashabiki na wadau wengine hatuoni lakini nao wanaishia kujadiliana kwenye vipindi blindly kama ilivyo kwenye vijiwe vyetu tu na hakuna jipya.
Wachambuzi wengi wanajitahidi maeneo mengi hasa analysis ya mpira waliouona lakini kuna vitu vingi sana hawajiongezi na kujikuta wana vitrend vinavyofanana sana.
Kwasasa mmefanikiwa kutengeneza nafasi yenu kwenye industry basi jitahidini kuongeza thamani kabla wadau hawajarudi kutumia watangazaji wa michezo kama ilivyokuwa zamani ambao wanaweza kuuza chai kidogo [emoji41]
Nyie mna vipaji na mmejikita huko kama wachambuzi, fanyeni analysis za mambo kwa undani badala ya kuwa na ufahamu kama sisi mashabiki.
Endeleeni na kazi nzuri na mjiongeze kidogo kulinda kiwanda chenu.