Huo mfano wako hausadifu hiki ninachokisema hapa. Simba, Yanga, Al-Ahly na mamelodi ni timu ambazo ziko robo finali ya CAF champions, hii inatosha kumfanya mchambuzi mwenye akili kuwa hizi timu uwanjani ziko na ulinganifu hata kama kwenye uwekezaji (pesa na majengo, miundombinu) zimezidiana sana. Kama ni swala la kuwekeza tu ziko timu ambazo zimewekeza sana kuliko simba na yanga lakini hazifika hatua hii ya robo finali, hivyo Kwa mchambuzi mwenye utimamu wa mwili na akili ingetosha kuondoa factor ya uwekezaji na kubakiza factors za upambanaji kiwanjani, teamwork, mbinu za mabenchi ya ufundi na mchango wa mashabiki uwanjani.
Huo mfano wako wa Man city na RB Leipzia ni mwendelezo wa ukosefu wa weredi kwenye uchambuzi kwakuwa Man city na RB haziko zote kwenye robo final ya EUFA champions kama zilivyo simba na al-ahly.
Ukiona mchezaji anacheza Afrika kiwango chake bado ni cha Afrika tu, wachezaji bora duniani wamenyakuliwa na timu za Ulaya, timu zetu za Afrika zina wachezaji wanaolinganalingana na kuzidiana tu viwango vya kujituma, motivation wanazopewa (pesa, mazingira na mabenchi ya ufundi).