Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Umeona ulichoandika hakina uhalisia? Hujui mpira, unataka Simba
Ukichepuka kidogo unapigwa.Kwahiyo Kuna timu inacheza bila kufuata maelekezo ya coach?
UmeelewekaNimeshuhudia dereva wa lori akichomolewa na kupigwa na dereva wa bodaboda baada ya dereva wa lori kumsukumia mtaroni dereva wa bodaboda.
Sio kwamba timu ikiwekeza sana lazima mara zote iifunge timu yenye uwekezaji mdogo. Wachambuzi wetu wanazilazimisha Al-Ahly na Mamelodi izifunge Simba na Yanga kwenye mashindano ya CAF champions eti kwakuwa zina uwekezaji mdogo kuliko al-ahly na mamelodi. Uchambuzi wa aina hii hauonyeshi weledi. Wachambuzi wanasahau factors za muunganiko wa timu, ari za wachezaji (self motivation) na uzuri wa mabenchi ya ufundi ya kila timu.
Ni kweli uwekezaji wa lori ni mkubwa kuliko uwekezaji wa bodaboda na ni kweli lori linapoigonga bodaboda mara zote lori litaiharibu zaidi pikipiki, lakini sio kweli kwamba mara zote dereva wa lori ana nguvu zaidi kuliko dereva wa bodaboda.
Timu zote zina wachezaji waliozifikisha timu zao robo finali, Pale uwanjani wanacheza wachezaji (madereva) sio pesa (malori na bodaboda).
uchambuzi usiokuwa na weledi unatia aibu. Yanga ina wachezaji hatari sana ila kwasababu za usimba na uyanga wachambuzi wanawachukulia poa sana. Tuna wachambuzi ambao hawashangai kwanini Yanga ina wachezaji waliocheza finali ya CAF champions, waliowafunga TP Mazembe, Club Africane, Rivers, Mediama, CRB, Simba goli 5 na kutoka sare na Al-Ahly. Wachambuzi uchwara wanaona yote hiyo ni kubahatisha tu badala ya uwezo mkubwa wa wachezaji. Walipotoka sare na mamelodi ndio kwanza wanaanza kuzinduka usingizini ingawa hata hivyo wanaona eti Yanga ilipaki bus ndio maana mamelodi haikupata goli. Huu ni umbumbumbu tu wa kukosa weledi kwenye kazi wanayoifanya.Umeeleweka