Wachambuzi wetu wanachumbua dereva wa bodaboda apigwe na dereva wa fuso

Umeeleweka
 
Umeeleweka
uchambuzi usiokuwa na weledi unatia aibu. Yanga ina wachezaji hatari sana ila kwasababu za usimba na uyanga wachambuzi wanawachukulia poa sana. Tuna wachambuzi ambao hawashangai kwanini Yanga ina wachezaji waliocheza finali ya CAF champions, waliowafunga TP Mazembe, Club Africane, Rivers, Mediama, CRB, Simba goli 5 na kutoka sare na Al-Ahly. Wachambuzi uchwara wanaona yote hiyo ni kubahatisha tu badala ya uwezo mkubwa wa wachezaji. Walipotoka sare na mamelodi ndio kwanza wanaanza kuzinduka usingizini ingawa hata hivyo wanaona eti Yanga ilipaki bus ndio maana mamelodi haikupata goli. Huu ni umbumbumbu tu wa kukosa weledi kwenye kazi wanayoifanya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…