Wachawi kutumia janga la corona kuumiza watu

Mdaiwa-Sugu

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
284
Reaction score
912
Wakuu tukiwa tunaendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga na corona kwa kuzingatia maelekezo ya wataalamu wa afya tukumbuke pia kuchukua tahadhari ya kujikinga na corona dhidi ya imani za kishirikina

Wachawi hupenda kutumia majanga ya mlipuko kama hili la corona kuumiza watu na kuwageuza misukule kwa lengo la kuwafanyia biashara(kuwauza) kwa matajiri na kuwafanyisha kazi mbali mbali zikiwemo za mashambani

Hii imewahi tokea kwenye moja ya kijiji huko kanda ya ziwa. Kulitokea mlipuko wa kipindupindu, wachawi wakajiongeza, wakaanza kuumiza watu na kuwageuza misukule kwa kile kilichodaiwa wanakufa kwa kipindupindu kumbe sivyo..Mpaka chezo lilipogundulika tayari baadhi ya watu walikuwa wameumizwa kwa njia hiyo..

Na vile serikali imesema mazishi yafanyike na watu wasiozidi kumi, imewarahisishia kabisa wachawi kutimiza adhima yao bila chezo kujulikana

Wakuu, corona ipo na inaua ila siyo kila kifo chanzo ni corona vingine chanzo kinaweza kuwa imani za kishirikina

Tuchukue tahadhari uchawi upo
 
Namuwekea Seat ya mwanzoni Mshana Jr
Aisee.. Basi ngoja niseme neno... Wachawi pamoja na kusemwa vibaya lakini ni watu wanaothamini sana ubora
Mchawi haaguzi broiler
Mchawi hachukui pesa mbovu wala iliyochanika
Mchawi harogi mgonjwa
Mchawi harogi mlemavu
Mchawi hali ndaza(viporo)
Mchawi hachukui damu iliyogganda

Jr[emoji769]
 
Mkuu Mshana Jr sikumaanisha mchawi anaroga mgonjwa ninachomaanisha hapa wachawi wataanza kuroga watu wazima ila kisingizo cha ugonjwa kitakuwa corona
 
Ndivyo mlichokubaliana kwenye kikao chenu mkuu?
 
Kwahiyo Hata Spain, Itary Na Us Wachawi Ndio Walichukua Watu? Jaman Chukueni Hatua Za Kujikinga Jamani Propaganda Zingine ndio maana mnakimbia kujifukiza na mnazidiwa.
Mkuu unafikiri uchawi upo Africa tu? Kama unafikiri spain, italy na US hamna uchawi unajidanganya. Uchawi upo kila sehemu mkuu
 

Ni kweli, inawezekana baadhi ya watu waliofariki, ndugu wakienda kufukua makaburi baada ya muda wanaweza kukuta migomba, magogo, etc., Kama huelewi haya Tanzania huijui vizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…