Wachawi kutumia janga la corona kuumiza watu

Wachawi kutumia janga la corona kuumiza watu

Watu watachukulia masikhara ila huo ndio ukweli wenyewe

Ndio maana watu wazito zaidi hata uso hawataki kutoa, kwa sababu kama walikuwa kwenye list ya wanted ya wachawi, wakijichanganya tu wachawi wanavumisha upepo kuelekea walipo. Hasa wale wanaotumia na kutegemea nguvu za giza, wachawi sasa ndio muda wao wa kufanya retaliation.
 
Itabidi ujifunze ulimwengu huu baadaye utajua kuwa kuna mambo ya ajabu sana yanayoendelea, hadi wakati huo ufike utakuwa umechelewa.
 

Attachments

  • 1588333255555.png
    1588333255555.png
    108.8 KB · Views: 4
Wakuu tukiwa tunaendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga na corona kwa kuzingatia maelekezo ya wataalamu wa afya tukumbuke pia kuchukua tahadhari ya kujikinga na corona dhidi ya imani za kishirikina

Wachawi hupenda kutumia majanga ya mlipuko kama hili la corona kuumiza watu na kuwageuza misukule kwa lengo la kuwafanyia biashara(kuwauza) kwa matajiri na kuwafanyisha kazi mbali mbali zikiwemo za mashambani

Hii imewahi tokea kwenye moja ya kijiji huko kanda ya ziwa. Kulitokea mlipuko wa kipindupindu, wachawi wakajiongeza, wakaanza kuumiza watu na kuwageuza misukule kwa kile kilichodaiwa wanakufa kwa kipindupindu kumbe sivyo..Mpaka chezo lilipogundulika tayari baadhi ya watu walikuwa wameumizwa kwa njia hiyo..

Na vile serikali imesema mazishi yafanyike na watu wasiozidi kumi, imewarahisishia kabisa wachawi kutimiza adhima yao bila chezo kujulikana

Wakuu, corona ipo na inaua ila siyo kila kifo chanzo ni corona vingine chanzo kinaweza kuwa imani za kishirikina

Tuchukue tahadhari uchawi upo

Mtoa mavi sikubaliani na hoja yako.

Sorry mods badilisheni. Sio mavi ni mada.

# Stay safe

# Stay home
 
Inasikitisha sana...

Kwa hiyo sasa tunaanza kusingizia na wachawi pia...



Cc: mahondaw
 
  1. Tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara
  2. Kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi
 
Aisee.. Basi ngoja niseme neno... Wachawi pamoja na kusemwa vibaya lakini ni watu wanaothamini sana ubora
Mchawi haaguzi broiler
Mchawi hachukui pesa mbovu wala iliyochanika
Mchawi harogi mgonjwa
Mchawi harogi mlemavu
Mchawi hali ndaza(viporo)
Mchawi hachukui damu iliyogganda

Jr[emoji769]
Na mwisho kabisa uchawi haupo
 
Aisee.. Basi ngoja niseme neno... Wachawi pamoja na kusemwa vibaya lakini ni watu wanaothamini sana ubora
Mchawi haaguzi broiler
Mchawi hachukui pesa mbovu wala iliyochanika
Mchawi harogi mgonjwa
Mchawi harogi mlemavu
Mchawi hali ndaza(viporo)
Mchawi hachukui damu iliyogganda

Jr[emoji769]
Please check your in box

"corona ipo tuchukue tahadhari"
 
Nakuunga mkono mtoa mada, hilo la kipindupindu niliwahi kulisikia huko kanda ya ziwa, hadi kipindi cha kiangazi na pengine siyo msimu wa maembe kipindupindu kinakula vichwa......saa hizi kila kifo atasingiziwa korona, hata kama kuna ulozi au sumu imetumika...
 
Back
Top Bottom