Hehehee! Hiyo kitu imeshanitokea mara kibao mpaka nikaamua kufanya utafiti. Haina uhusiano wowote na uchawi kama watu wengi tunavyofundishwa (siingilii imani za watu). Inaitwa Sleep Paralysis. Kinachotokea ni kwamba, subconscious part of the brain inakua kwenye ndoto (kumbuka hii ndio ina control movements za viungo wakati ukiwa usingizini) halafu ghafla the conscious part of the brain inaamka.
Sasa kimbembe ni kwamba, ukakua kwenye ndoto, mara nyingi za kutisha, then unapata fahamu wakati mwili bado uko ndotoni, unataka kufanya movement hauwezi. Unatamani kupiga kelele haitoki. Basi inakua taabu tupu. Ila inakaa muda mfupi (ranging from seconds to minutes).